Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Kabla ya kuacha kazi anza hio miradi japo kwa 40% kwa mwaka mmoja then pima upepo faida na hasara ipo vipi?
 
Usipigie hesabu pesa iliyo mfukoni mwa mwenzio utashangazwa. mifuko ya uhifadhi ya jamii ndio inayofanya watu wanakufa mapema, usitegemee pesa Kule.
 
KILA la kheri ndugu angalia motivation speaker wasikuharibie future
 
Ila siku Mimi nitakapoamua kuachana na ajira sitotangaza kwa mtu yeyote Ni kimya kimya watu watashutukia tu sipo .

Sometime outside energy zinaleta gundu .



Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Ni kweli Mkuu, ukitaka kufanya jambo usiseme sababu wengi wao wanaiogopa hio hali unayoenda kupitia, Lazima wakukatishe tamaa, amka mwenyewe watakukuta mbele mbele huko.ukisubiri uambiwe na watu wengine shetani ataitumia hio nafasi kuharibu mipango yako.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Vizuri ila usimtegemee saaana huyo mtu.
 
Huyu atakuja tena kuomba ushauri namna ya kurudi kazini.

Tuendeleee na kazi,mwacheni.
Lakini uweke akiba ya maneno mkuu maana unaweza jikuta unakuja kuomba kazi kwake baada ya miaka kadhaa. Mfano miaka hiyo akina Kitenge walikuwa hawapigi nyimbo za Domo wakiwa ITV lakini sasa hivi Domo ndio kawaajiri na awaweka mjini kupitia WASAFI TV. Maisha yanadunda mkuu hata kama unakomaa kwenye ajira.
 
Au anza kilimo cha matikiti kama motivesheno spika wengi wanavyo shauri
 
Kuwa makini mkuu ushauri wangu usiache kazi fanya kazi huku umejiajiri kwa maana maisha ya sasa ni magumu sana kuliko miaka ile ya 90 tuliokuwa tunasoma. Mfungulie mkeo kile kitu anachokipenda kutoka moyoni siyo wewe unachokipenda ila yeye kaa chini uongee naye atakachokuambia kwamba ni ndoto yake mfungulie ila wewe usiache kazi ila na wewe jiajiri weka mtu shamba pamoja na kukuangalia shamba na mifugo na huku mkeo umemfungulia kile akipendacho yeye na huku wewe unatumikisha angalau hata miaka mitatu mbeleni unaangalia shamba na mifugo vinakwendaje na mkeo naye anakwenda vizuri kama mambo yanakwenda vizuri sana ndiyo sasa unaomba kuacha kazi kwa kuwa shamba na biashara ya mkeo vyote vimekua yaani mwendo wa faida kwenda juu.
 
Kama ajira inakulipa vizuri bora ukomae hapo hapo.

Hizi mambo za kukimbilia kufuga kuku utajikuta umepoteza kila kitu hadi huyo mwanamke.

Niko sahii kurekebishwa
Ukiwa na fikra ya kupata faida mwanzo tu baada ya kuanza biashara au ufigaji....hii itakula kwako
Kila jambo linahitaji utulivu,subra,mikakati nk
Hakuna atakaekufa na njaa(ukiwa sehemu ya amani) ikiwa ni mpambanaji
 
Shukran sana kwa ushauri wako
 
Anza kufuga huku upo kwenye ajira usidhan biashara itakupa faida haraka haraka anza taratibu mpaka biashara ikomae
Biashara hazielewekagi
Ushauri mzuri sana mkuu huo! Asiache kazi kabla hajasimama! Ingawa changamoto ninavyoona kwa huyo mdau ni mtaji maana anataka mafao ndiyo ayatumie kama mtaji!
 
Kufuga nguruwe ✔
Kufuga kuku✔
Kulima nyanya za kumwagilia❌🚫
Kununua mazao na kuyauza ✔

Tafadhari usiweke life savings yako kwenye kilimo cha mazao yanayo oza kama nyanya.
Nyanya kichaa kalime hizo kwa kujifurahisha ukiwa umetoboa maisha kwenye ufugaji au biashara zingine.

Kama una mtaji mzuri na unamapenzi sana na nyanya kanunue mashine na vifungashio usindike na kuuza nyanya ulizo ongeza mnyororo wa thamani ambazo zinakaa kwenye shelves miaka au miezi kibao bila kuoza.
 
Mku sikushauri hata kidogo .Tafuta likizo tumia hizo pesa kuanzisha mradi ukiwa kazin, Tafuta kijana mwaminifu hapo unatumia mshahara kuendeshea mradi mradi ukiweza kusimama ndio uache kazi.
 
Kama mwezi haukutani ni bora ukalime tu aisee, kuliko kumfaidisha muajiri
 
bro hao PSSSF huwa wanazingua kutoa helaaaaa!
UWE NA UHAKIKA KABLA YA KUTEMA KAZI
 
Haya maisha wakati mwingine inabidi ujilipue tu. Wenye Kiingereza chao wanasema (risk taking). Vinginevyo ukiwa mwoga utabaki umedumaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…