Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Kila la kheri mkuu, naimani utaenda kufanikiwa.....cha msingi tu ni kiziba masikio kwa watakaokukatisha tamaa
 
Mkuu!Kitu rahisi kukimudu ni wewe utafute kijiji chenye uhitaji wa mashine ya kukoboa na kusaga mahindi.Nunua eneo ambalo umeme njia tatu umefika na uweke mashine.Mzee kila mwezi utaendelea kupata mshahara kwa mashine yako.Ukiweza saga mwenyewe,hakika hutajuta.
 
Acha kazi baada ya kuanzisha mradi na kuona unafanya vizuri. Sio uache kazi na kuanzisha mradi.
Wazo lako ni zuri,changamoto iliyopo ni kupata huo mtaji wa kuweza kuwekeza ndio maana nimeona njia sahihi ni kuacha kazi ili nichukue mafao yangu.
 
Nyanya, ninyanyue, nyanya ni nyanyase, kideri plus homa ya nguruwe, mahindi kushuka bei, jipange jibaba, though u had a guts
 
Mmmmmh!Huu mchongo nimeutamani.Vp kama mimi nitaamua kujafanya hii kitu lakini nikiwa mbali,naweza toboa?.
 
Plan b ipo,nimeandika kuwa nitamfungulia wife biashara pale nyumbani maana kuna nafasi ya kufanya hivyo..
Wakati uno porini huko unamenyeka na jembe na kufuga nguruwe, biashara uliyomfungulia mkeo nyumbani haitakuwa salama.....

Mkeo watamla, pesa atahonga, na biashara itakufa arif, we kama vp beba huyo mkeo mwende wote huko chaka hiyo m2 uliyotaka kuichoma ikaongeze mtaji huko uendako

Sioni sababu ya kumuacha mkeo nyumbani apigwe mashine na wahuni wkt ww ukiwa huko vichakani ukitafuta pesa,.....

Mwanamke sio wa kuacha mbali arif, hata shetani alimdanganya hawa wakati Adam akiwa hayupo, take care
 
Mkuu nikushukuru kwa dhati kabisa kwa huu ushauri.
Mkuu nami naamini kabisa kuwa maendeleo huchukua muda,sio swala la mda mfupi na nilitamni nianzishe mradi nikiwa bado niko kazini ila changamoto ni kwamba mshahara unaishia kwenye ada,chakula na nauli tena muda mwingine nakopa so mwisho wa mwezi ukifika unakuta pesa yote inapukutika.

Kampuni ninayofanya inatoa mikataba ya mwaka mmoja mmoja kiasi kwamba tunakosa sifa ya kukopesheka katika taasisi za kifedha,ingekuwa inatupa japo hata miaka 4 tungekopesheka na ningeutumia huo mkopo kuanzisha uwekezaji.

Sasa kutokana na ushauri wako pamoja na wadau wengine ambao wamenitahadharisha kuwa huenda mafao yasitoke mapema kama ambavyo nafikiria na muda huo nitakuwa sina kazi itasababisha niishi katika mazingira magumu zaidi...

Siwezi kupuuza ushauri hata kidogo ndio maana nimelileta hapa ili niweze kupata msaada katika kufikia malengo yangu...
kwa kuzingatia hayo yote nimeona nifanye maamuzi mengine ili niweze kupata mtaji wa kuandaa mazingira ya uwekezaji..

Mwakani watoto wangu wawili niwahamishe shule za kulipia niwapeleke za kawaida,halafu huyu mmoja aliyeko la sita nimwache amalize la 7 maana yeye kwa sasa haiwezekani na sekondari atasoma za kawaida, then kile kiasi nilichokuwa nakilipa kama ada ndio nikitumie kuwekeza hapa nyumbani.
 
mimi binafsi sikushauri kuhusu kuku,nafuga kuku ndo maana nakupa ushauri.

Ili uweze kupata faida hiyo unayotaka itakubidi ufuge kuku kuanzia 500 na kuendelea iwe ni wa kisasa,chotara au kienyeji hivyo chakula kimepanda bei hakuna mfano kuku wengi hivyo huwez sema wakajitafutie chakula(kienyeji na chotara)wakashiba lazima uchanganye uwape na mara nyingi wakiwa vifaranga uwape cha dukani ili wapate mwili haraka ndo unaanza kuchanganyA.

Labda nguruwe na kilimo ila kwa sasa kuku ni uwe na pesa ya maana na si yamawazo kwenye kuwalisha.
 
Nashukuru kwa ushauri mkuu,nitaufanyia kazi
 
Kuna mzee mmoja ofisini hua ananiambia haya na kunisistiza kutokupoteza muda kazini na kuanza kuwekeza kwenye kilimo na biashara
 
Ushauri mzuri sana mkuu huo! Asiache kazi kabla hajasimama! Ingawa changamoto ninavyoona kwa huyo mdau ni mtaji maana anataka mafao ndiyo ayatumie kama mtaji!
Nawatoa watoto shule za kulipia ili nipate kukitumia kile kiasi cha ada kuanzisha miradi.
 
Ni muhimu kusoma upepo na namna hali halisi ilivyo
Kuwa makini sana kayika kutanya maamuzi yako hasa kama haya ambayo ndio muhimili na mustakabali mzima wa maisha yako ya kiuchumi

Katika ujasiliamali kwa asilimia kubwa ya waliofanikiwa ni wale wenye walau miaka mitano na kuendelea katika sekta hiyo kama uko tayari kusota miaka zaidi ya sita na katika hali tofautitofauti sawa

Lakini kujiajiri kuna raha yake ila unatakiwa kuwa na akili ua matumizi ya pesa aisee
 
Nimekusoma mkuu.
 
Sawa kabisa kuhusu issue za shule za watoto. Vipi kuhusu mkeo? unamtumia vipi katika uzalishaji wa pato la familia? Kumwacha awe mama wa nyumbani bila shughuli yoyote ni kosa kubwa linalochangia kuanguka kwenu.

Mtengenezee mradi mdogo wenye kutumia mtaji mdogo ili ajifunze ujasiliamali. Mke ni nguvu kazi tosha sana ambayo ikifanikiwa utapata amani ya moyo.

Option nyingine ni wewe kama wewe kujiendeleza kielimu ili upate maarifa zaidi yatakayokupa kazi nzuri ambayo itakupa mtaji wa biashara. Hilo ni wazo la muda mrefu sana ambalo kama huna haraka unaweza kulifanyia kazi.

Jaribu kuyaandika maisha yako unayotaka kuishi na mipango ya kufanikisha hayo malengo na dira yako. Hauna mtaji so ukiingia kwenye hiyo mipango ya ujasiliamali bila mtaji na kuacha kazi itakuwa anguko kubwa sana kimaisha. Kaa chini andaa plan ya maisha ya muda mrefu kisha tafuta njia za kupita ili ufike unapopataka.

Nakupa mfano wangu binafsi, baada ya kuajiriwa nilitaka kuwa na cheo na pia kuwa na uwezo hivyo nikajiwekea malengo kuwa ili nipate cheo lazima nifanye kazi kwa bidii, kujituma na kuongeza elimu. Nikayafanyia kazi hayo katika kipindi cha miaka mitano nikawa na elimu ya kutosha na cheo kikapanda. Baada ya hapo nikawa na uwezo wa kukopa parefu na pia posho zikawa nyingi ndio nikaanza ujasiliamali na uwekezaji

Imenichukua miaka 15 kufikia kuwa mfanyakazi mwenye cheo na mjasiliamali. Siongei kwa kujisifia ila nakupa hamasa ili upitie njia sahihi ambayo mara nyingi uwa ni ndefu

Kaa chini chora ramani ya maisha yako halafu anza kufanyia kazi mpaka ufikie unapotaka. Bila kuwa na dira sahihi utapotea mazima. Naona kama una haraka kwa kuangali mwenzako amefanya nini. Kila mtu ana njia yake ambayo amepiga hesabu zake vizuri
 
Kama ajira inakulipa vizuri bora ukomae hapo hapo.

Hizi mambo za kukimbilia kufuga kuku utajikuta umepoteza kila kitu hadi huyo mwanamke.

Niko sahii kurekebishwa
Hapo kwenye kupoteza hadi Mwanamke------ JF kiboko kabisaaaaaaaaaaaaa
 
Well said,
Mradi nitakaouanzisha nyumbani ni kwaajili ya wife kuusimamia so hatokuwa tena hana shughuli ya kufanya mkuu.
kuhusu elimu niko na degree ya elimu,nimeipata chuo kikuu huria na kuhusu kazi yangu sio mbaya sana kwani take home yangu 700,000/
Plan ya aina ya maisha niyatakayo ninayo na ndiyo imekuwa ikinisumbua sana namna na ya kuifikia...na hii imetokanana na ukweli kwamba sikutaka wanangu wasome shule za kawaida na huko ndiko pesa zangu nyingi zinakokwenda mkuu.

Kwakuwa nimeamua kuwatoa ni matumaini yangu taratiibu nitaianza safari kuelekea uhuru wa kipato.

Mkuu nakushukuru sana kwa in put yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…