Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Ewe mpenzi wa soka la Tanzania, habari zikufikie popote ulipo kuwa kikosi cha Simba SC kimeanza vizuri katika maandalizi yake ya Msimu mpya huko nchini Misri. Hii ni baada ya kukichapa kikosi cha El Qanah siku ya jana baada ya kuibuka na ushindi mnono wa goli 3-0 (Tatu kwa mtungi).
Wale wote mnaobeza kuwa kikosi cha Simba kimepimana nguvu na timu ndogo ya daraja la 2 mnakumbushwa kuwa soka ni taaluma. Kwa ugeni ule wa wachezaji na kocha akiwa mgeni huku akikisuka upya kikosi hiki mlitegemea mechi ya kwanza aanze kucheza na Al Ahly?
Kwa maoni yangu naona Management ya Simba inafanya kazi professionally maana ni muhimu sana kuwajengea confidence wachezaji katika hatua hizi za awali, confidence yenyewe ndio hiyo ya kuanza taratibu kwa ushindi. Hivyo baada ya hapo tutegemee Simba kukichapa na Timu kubwa kubwa. Hebu mkae kwa kutulia.