Huu ni uchuro au Mungu anasema na mwanakijiji kuwa Kijiji kijiandae kwa lolote?

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
1,458
Reaction score
617
Leo nimebahatika kupigiwa simu na rafiki yangu wa siku nyingi sana wa kijijini akanisimulia kisa na kuniuliza maswali ambayo sikuwa na Majibu.

Kijijini kwao kiongozi weo alikuwa anaitwa Kifungo, na katika safu yake kulikuwa na Viongozi wengine ambao ni Makubaliano, Kibarua, Kitochi, na wengine. Baadae Kifungo alifariki, na baada ya kufariki nafasi ile akachukua msaidizi wake anayeitwa Makubaliano, Baada ya makubaliano kuchungua Uongozi akapendekeza asaidiwe na Mr Mradi na ikawa hivyo, (Kibarua na Kitochi wakaendelea kuwepo pia).

Kuna siku Kibarua alijitoa kwenye uongozi wa kijiji japo inasemekana alitolewa, sasa baada ya kutolewa akachaguliwa Shwari achukue nafasi ya Kibarua na ikawa hivyo.

Muda wa uongozi ulipokaribia kuisha Makubaliano akasema yeyeanataka kuendelea kama wanakijiji watamridhia aendelee ila mwenzie Mradi akaomba apumzike, hivyo Makubaliano akampendekeza Bwana Imani awe msaidizi mpya.

Baadae pia Kiswaswadu akasema yeye haendelei, anapumzika.

Baadae Kibarua alikuja akafariki ghafla. Sasa toka Kibarua amefariki huyu ndugu anasema mapaka yanalia sana na anaota ndoto za ajabuajabu sana, anaona kama kijijini kwao wataandamwa na mikosi maana sasa ni kama uchuro.

Sasa swali aliloniuliza, je, ikitokea ghafla makubaliano anaumwa na Imani anaumwa kias kwamba hakuna anayeweza kusimama na kufanya mkutano wa kijiji wala kufanya maamuzi, je hali itakuwaje kwa kijiji na wanakijiji?
 
Umesahau kiswaswadu alisema kwenye mkutano wa kijiji kwamba ntaendelea na shughuli za kijiji lkn ghafla akaghairi akaema napumzika hatujui mpk leo kwann apumzike wakat alitamka kwenye kikao cha VDC kwamba ataendelea au kuna mpango wa kufanywa mwenyekiti wa kitongoji kwa hadhi yake ingekuwa sio poa
 
Aiseee changamoto basi labda maamuzi yatasitishwa na mradi akae hapo alafu apange tena maamuzi wakati mwingine
 
πŸ˜‚πŸ˜‚Kwa kweli hii Fasihi nimekuelewa nizaidi ya Shabani Robert na Ngugi wa Thiongo Kwani Mr Mradi huko likizoni sijui mapumzikoni hajaanzisha Mradi wowote wa UjasiriamaliπŸ˜‚? Au anataka aendelee kufundisha wenzake miradi?
 

Kuna mashahidi wa kificho siku hizi

Jichanganye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…