Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
Diwani wa Nkiwanzenzaa
Asiyejuwa katiba, kanuni, ilani, miongozo, na taratibu. Mwenye elimu ya moja, mbili, tatu Siiiii mzuka. Amesusiwa kikao baada ya kutaka kupandikiza watu kwenye SSEEM kama alivyopandikizwa yeye kwa rushwa kwenye udiwani.
Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho nikikemea tabia mbovu na chafu inayoota mizizi ndani ya SSEEM ya kutumia fedha na hisia binafsi kukiendesha chama, nikaanza. WanaSSEEM wengi wanadhulumiwa haki zao za kimsingi kwa sababu ya kukosa uelewa na kuwa na uoga wa kusimama kutetea haki zao.
Niwaombe wahusika; uongozi maana yake ni kushughulika na kero za watu. Viongozi mnaohusika na kusimamia haki, tendeni haki bila muhali. Acheni kuona machozi ya watu wakilia huku mliopaswa kuchukua hatua mkicheka, kisha mnasimama kuhubiri haki msiyoipenda kuupigania.
Wakili Jasiri na Msomi Boniface Anyisile Mwabukusi, Rais wa TLS, nakumbuka tarehe 05/10/2024, alisema:
Tusipende kuona machozi ya mwananchi mwenzetu akilia mbele yetu kwenye jambo tunaloweza kutatua.
Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Nzabayanga Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania, akiwa Arusha tarehe 11/05/2023, alisema:
TLS na taasisi zingine za sheria (kwa pamoja) tunao wajibu mkubwa katika utoaji na upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Mwisho wa kunukuu.
Tunapaswa kusimama na kusema kuwa hisia binafsi bila kufuata sheria basi. Tusipokemea, tunazidi kuwaumiza wanyonge kutokana na utapeli unaofanywa na baadhi ya viongozi matapeli wenye kutumia rushwa wasiothamini sheria na kanuni.
Kuna nafasi tatu wazi katika Halmashauri ya SSEEM, kata ya Nkiwanzenzaa. Zinatakiwa kujazwa na makada wafia chama wenye kujuwa ilani, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu za SSEEM.
Sasa, diwani wa Nkiwanzenzaa kwa vile anaona kila kukicha anapoteza mivuto wa kukubalika, akaona atumie fursa hii atafute manyangalagata ya kuokoteleza yasiyojuwa lolote kuhusu chama ayapachike kwenye halmashauri ya kata ili kuongeza wingi wa sauti za ubwabwa wali nazi za "Ndiyooooooo! Muzeeeee!"
Kawaida kabla ya uchaguzi wa wajumbe wa halmashauri ya kata, huwa kuna vikao vya awali: Kamati ya Maadili ya Kata kuangalia mifumo ya wanaSSEEM isivizwe, kamati ya siasa ya kata. Ndani ya kata ya Nkiwanzenzaa haya hayafuatwi. Watu wanasikiliza amri kutoka kwa diwani. Akisema kushoto ni kushoto, kulia ni kulia.
Iko hivi:
Mchakato ndani ya Nkiwanzenzaa baada ya majina kurudi kutoka wilayani Hilyalyoh yakapelekwa kwa diwani asiye na elimu, mwenye kutumia amri. Akakiambia chama, hakuna kuweka vikao, "Mimi nina watu wangu, hawakijuwi chama cha Mapandyunzye. Mtawafundisha baadaye ila kwa sasa wakateni wanaSSEEM wafia chama, wekeni maboya yangu haya."
Wajumbe woote wa kamati ya siasa ya kata ya Nkiwanzenzaa wakashangaa. Wakaona dhamira ya wazi ya diwani kukiuwa chama na kuneemesha nduguze anaowachukuwa kutokea kuleeee kyafyu. Wajumbe wakagoma, ikabidi katibu wa wilaya apigiwe simu na akatoa tamko uchaguzi usitishwe.
Anaenda leo huko Nkiwanzenzaa kujionea na kusikiliza haki za wanaSSEEM mafukara zinavyokanyagwa na diwani mpenda vyeo, asiye na elimu, mshirikina mwenye kutumia unyonge wa wanaSSEEM kama kisa cha kuwalisha ubwabwa na kumfanya adumu madarakani akiwa haulizwi mapato wala matumizi, akijineemesha kwa kutumia uelewa duni wa mafukara wala ubwabwa wasiojuwa sheria kuhusu haki zao.
Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Nzabayanga Mpango, akifungua mkutano wa TLS akiwa Arusha tarehe 11/05/2023, alisema:
Wapo watu wengi wamepoteza haki zao kwa kukosa uelewa wa sheria.
Mwisho wa kunukuu.
Tutoe elimu bila kuchoka ikiwa ni pamoja na kuanika mauozo kama haya ili watu wajielewe, wasiburuzwe.
Nikashtuka ndotoni nikiwa kimya.
Kidumu chama cha mapinduzi.
Mathias Mugerwa Kahinga