SI KWELI Huu ni ukurasa wa Humphrey Polepole kwenye mtandao wa X

SI KWELI Huu ni ukurasa wa Humphrey Polepole kwenye mtandao wa X

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
photo_2025-09-03_16-02-34.jpg
 
Tunachokijua
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye ambaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.

Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram alichapisha barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba na baadaye tarehe 18, Julai 2025 alifanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alikosoa utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema 'Wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Mchakato wa kupata wagombea tumeukosea'

Agosti 05, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Katika mtandao wa X, upo ukurasa unaotumia utambulisho wa Humphrey Polepole ambapo kuanzia mwezi Julai 2025, ambao umekuwa ukichapisha taarifa mbalimbali kuhusu mwanasiasa huyo.


Je, huo ni Ukurasa halisi wa Humphrey Polepole?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Ukurasa huo katika mtandao wa X zamani Twitter ulitengenezwa mnamo mwezi Mei 2014. Lakini ukurasa huo unaonesha taarifa zilizopakiwa kuanzia mwezi Julai 2025 ambapo nyuma ya hapo hakuna taarifa yoyote inayoonekana.

Aidha Polepole mwenyewe amethibitisha kutohusika na ukurasa huo kwani hajajiunga kabisa katika mtandao wa X. Hivyo ni muhimu kuwa makini na maudhui yanayotolewa na Ukurasa huo kwa utambulisho wa Polepole kwani mwenyewe hahusiki nao.

Kurasa Rami ambazo amekuwa akizitumia ni pamoja na ule wa Instagram na Facebook.​
Anaenda na upepo tu, parody
 
Back
Top Bottom