Huu ni ulimbukeni wa kiwango cha juu sana. Tangu lini mchezaji akatambulishwa kwenye mkutano wa uchaguzi?

Katambulishwa kwa wapiga kura, kapiga kampeni, lakini jamani kilichofanyika sio sawa hata kama unaipend timu vipi ilikuwa sio sawa.
Lakini wana haki ya kufanya lolote hata ni maamuzi ya wanachama , klabu yao imenunuliwa na wao maskini - atakalo fanya tajiri ni sawa tu.
Tena mengi yanakuja haya huenda nafuu.
 
Mboa sisi Simba tunateseka.

Yanga wana Rais wao wamemchagua kwa kura, sisi Simba tuna Rais wetu tena tunamwita wa Heshima ambaye tumempa hajapigiwa kura.

Sasa yupi hapo wenye timu ni mbunbumbu?
 
Inabidi tuwashinikize viongozi wetu wa simba watuambie Shilingi 85 alizosema Boss Mo aliziweka jwenye Akaunti gani.

Kuna benki hapa Tanzania inapokea Shilingi 85?
 
Bwashee hiyo inaitwa mbinu za Medani au siasa za mpira😂😂, Aliyekuwa akitambulishwa pale ni MKANDARASI aliyekuwa akitambulisha. Kwamba kwa nini asipewe Urais hali kuwa ametuletea Mchezaji aliyetemwa ulaya😂😂. Bila kujizuia Msema ovyo akamtangaza kabisa aitwe Rais😂😂
 
Mboa sisi Simba tunateseka.

Yanga wana Rais wao wamemchagua kwa kura, sisi Simba tuna Rais wetu tena tunamwita wa Heshima ambaye tumempa hajapigiwa kura.

Sasa yupi hapo wenye timu ni mbunbumbu?

Yupi aliyepigiwa kura? Kura ya mtu mmoja si ni hadaa tu kama hadaa zingine ili kuhalalisha tu!
 
Hiyo ilikuwa ni ghilba na rushwa dhahiri kwa wapiga kura.TAKUKURU kamata,hoji,chunguza na fungulieni mashtaka hao matapeli waliofanya hivyo.
 
Acha kuteseka kwa vitu visivyo kuhusu. Maana utakufa kabla ya wakati wako.
 
Yupi aliyepigiwa kura? Kura ya mtu mmoja si ni hadaa tu kama hadaa zingine ili kuhalalisha tu!
Si ungeenda kuchukua fomu ya kugombea ili uchuane naye kwenye hiyo nafasi?

Na kama hukuwa na sifa, bas ni vizuri ukikaa kimya ili kuonesha una busara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…