Huu ni Utapeli au ndivyo Biashara inavyofanywa?

Kikubwa mwenye kitambulisho awepo.
Sio lazima awepo mkuu, hizi biashara tunazifanya kila siku hapa mjini.
Nikuulize swali je, kama mwenye kitambulisho atakuwa ameshafariki itakuaje?
 
Mkuu huyo mwenye gari sio lazima awepo ila hakikiaha una passport size picha zake namba ya simu na kitambulisho chenye jina sawa na jina la kwenye kadi. Lakini sababu una mashaka fanya naye mazungumzo kabisa huyo mwenye jina kwenye kadi.
Mbona mnapotosha jamani? Mwenye gari siyo lazima awepo? Kama aliuawa na kuporwa vitambulisho, gari na kadi yake na sasa majambazi ndiyo wanalipiga bei? Kitambulisho kina maana gani basi kama mwenyewe hatakiwi kuwepo ila ni kopi ya kitambulisho chake tu? NB: Hata kama ulishafanikiwa ku-register bila mwenye kitambulisho kuwepo ni kosa!
 
Sio lazima awepo mkuu, hizi biashara tunazifanya kila siku hapa mjini.
Nikuulize swali je, kama mwenye kitambulisho atakuwa ameshafariki itakuaje?
Kama amefariki kuna sahihi na halali za kuonyesha kuwa amefariki na mwenye kopi ya kitambulisho ndiye anatakiwa kuwa nacho. Narudia: hata kama ''hizo biashara'' mnazifanya kila siku lakini mnafanya kimakosa na kuna siku mtaingia kwenye matata.
 
Ipo hivi, utakapoenda TRA kufanya transfer mwenye kitambulisho hua lazima apigiwe simu ili kuconfirm kama gari ameuza au vp, so kama anamshaka anatakiwa waende TRA ili waconfirm kabla ya kufanya biashara.
 
Kama amefariki kuna sahihi na halali za kuonyesha kuwa amefariki na mwenye kopi ya kitambulisho ndiye anatakiwa kuwa nacho. Narudia: hata kama ''hizo biashara'' mnazifanya kila siku lakini mnafanya kimakosa na kuna siku mtaingia kwenye matata.
Na ndio maana huwa kuna mikataba pia mkuu, usifikir hizi biashara huwa zinafanyikia chini ya miti.
 
Hakunaga hiyo kitu. Title transfer huwa inafanyika na muhusika akiwapo. Hauwezi kubadili umiliki wa mali na muhusika hayupo. Na uwe makini sana wanaweza kukutengenezea fake documents wakakukutanisha na fake owner ukapelekwa kwa fake TRA officers.
 
Kuna jamaangu gari ipo imeshikiriwa TRA hadi sasa,
Ila kama wanaokuuzia huwafahamu,
Jaribu kuanzia TRA Kabla hujalipia,
Note" sio lazima mmiliki awepo.
 
Mkuu kama unanumua gari vitu muhimu ni picha ya passport, copy ya kutambulisho(uraia/Licence) na kadi og ya gari. Ukiwa na hizo doc kubadilisha umiliki ni chap tu
- Ongezea mkataba wa mauziano.
 
Kufanya transfer ni siku moja tu.
Mwambie ashughulikie.
Pili hakikisha unapewa na mkataba waliouziana
 
Tunapotosha kivipi mkuu. Nimesema apate mawasiliano na mwenye jina la kadi sasa kama unawasiliana nae si atakwambia kama aliibiwa? Nimeshafanya mara kadhaa hizi transfer pale TRA huwa wanataka mawasiliano ya mwenye gari anapigiwa simi sio lazima mwende nae sasa kama ningekuwa nakoseq nisingepata hizo transfer zote.
 
Uwepo wake unaweza kuonyeshwa kwa njia mbali mbali. Siyo lazima physically. Hata uwakilishi unaotambulikana kisheria. Cha muhimu ni ridhaa yake ipatikane kwa njia inayokubalika kisheria. Nilichokataa ni kuwa kitambulisho chake pekee kuweza kuwa ndiyo ridhaa yake kinapowakilishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…