Huu ni utofauti wangu kati ya KUFA, KUFARIKI na KUAGA DUNIA

Huu ni utofauti wangu kati ya KUFA, KUFARIKI na KUAGA DUNIA

Binafsi neno/msamiati KUFA nalitafsiri ni hali ya "umaalumu" ya kushindwa kufanya kazi kabisa, na miale ya tafsiri hii( kwangu ni mipana). Inahusisha viumbe vilivyo hai na vile visivyo hai( vilivyotengenezwa kwa kukamilisha kazi "maalumu")

Mfano1: kwa viumbe hai unaposema ame'KUFA' una maana ya kwamba zile biological function zote(umaalumu) zinazomfanya aendelee kuwa hai zimeshindwa kabisa kuendelea kufanya hiyo kazi.

Mfano2: kwa viumbe visivyo hai( hapa nazungumzia vitu vya kuyengeneza) kama vitu vya electronics na vinginevyo vilivyotengenezwa kwa kufanya kazi " maalumu" navyo, vikishindwa kufanya kazi yake kabisa iliyokusudiwa; binafsi natafsiri ya kwamba kime'KUFA'

Kwa mantiki hiyo, KUFA huwa nalitafsiri ni kushindwa kabisa kwa kufanya kazi "maalumu" kiwe kwa kiumbe hai au vitu vinavyotengenezwa kwa kazi husika. Kwa hiyo, hili neno linatumika kote kote kama mifano ya juu inavyoonesha.

Tukija kwenye KUFARIKI+KUAGA DUNIA kwa ufahamu wangu mdogo ni maneno yenye maana moja tena yenye kubagua, na kubagua kwake ni kwa viumbe hai tu na si viumbe hai vyote. Bali ni mmoja tu naye ni binadamu na limempa hadhi ya kumchagua yeye tu, kwa sababu binadamu ana ule upekee kwa viumbe hai kwa ujumla(ijapokuwa maneno yenyewe ni yenye kuleta majonzi). Kwa sababu huwezi kusema Kuku amefariki au ameaga Dunia. Ni kweli italeta maana lakini tutasema sentensi imekosa ile " Collocation " Vilevile inaonesha utajiri wa Lugha wa kuwa na maneno/misamiati mingi yenye kurejelea maana moja.

KUFARIKI/KUAGA DUNIA ni kanuni na nidhamu ya maumbile ya mwanadamu kufikia utamati wa mawasiliano ya kiroho, kimwili na kiakili. Kwa sababu tupo kwenye Sayari Dunia ndipo likapatikana KUAGA/ KUFARIKI DUNIA. Kama tungekuwa sayari ya Krypton basi tungesema KUAGA/KUFARIKI KRYPTON.

Additional point:

Ukija kiistilahi KUFARIKI kumetokana na neno "al faraqa" la kiarabu kwa maana ya tengana au kutengana. Kwa kiswahili linaongezewa nyama na kulingana na sentensi husika. Mfano; usilete m'faraka'no kwa maana usilete utengano. Kufariki ni Faraqa ukijumlisha Dunia inakuwa Al faruq bayna dduniya( kutengana na dunia) Waswahili wanasema kafariki Dunia.

Ni mtazamo wangu, ni ruhusa kunisahihisha.
 
Mimi nnachojua ni kuwa
KUFA - Huwa wanakufa Masikini.
KUFARIKI/KUAGA DUNIA - Huwa kwa Matajiri, Watu Maarufu na watu Mashuhuri!
 
Wasalaam JF members[emoji1538]

Moja kwa moja kwenye mada, ila kabla sijagusa mhimili wa mada niweke misamiati hii sawa kwa kiwango cha upeo wangu (siyo cha BAKITA)

Tafsiri ya haya maneno:

1. KUFA, binafsi naamini wapo wanadamu wanaokufa na wasiokufa. Kufa kwa tafsiri yangu ni roho kuukimbia mwili kutokana na uharibifu wa ghafla wa mwili utokanao ama na Ajali, Kupigwa, au Majanga asili mfano matetemeko au radi

2. KUFARIKI, hili linakaribiana sana na KUFA ila ni tofauti kimazingira. Hapa pia roho inaukimbia mwili. Ila tofauti hapa huwa si kutokana na uharibifu wa mwili bali hutokana tu na roho kuichoka hali ya mwili. Mara nyingi wanaofariki ni wagonjwa, watu waliopata njaa kali au waliokosa hewa. Yaani vile vitu vinavyoutesa na kuuchosha mwili basi utafariki

3. KUAGA DUNIA, hili kundi ndio linanishangaza kidogo katika tafakari yangu. Hapa inatokea roho inawasiliana moja kwa moja na baadhi ya viungo vya mwili hususa ubongo na kuupa taarifa kuwa sasa roho inaitaji kutoka na kwenda eneo tofauti. Hii ni hali ya bahati sana kutokea kwa mwanadamu. Je, umewahi kusikia watu wakisema "alijua atakufa akawa anatuaga" basi ndio hali hii. Tatizo ni moja tu watu hudhani mtu huyo kafa kumbe hajafa bali ameaga dunia.

Watu wa kundi hili mara nyingi huwa ni wazee au hata vijana na watoto, na hasa kwa uzoefu na fikra yangu huwa halii hii huwapata wale watu wakorofi na wenye misimamo yao.

POINT YA ZIADA:

KULALA: Umewahi kusikia habari za Yesu kristu au Nabii Issaa za kuwaambia waombolezaji kuwa "mtoto hajafa amelala tu!". Umekumbuka ee!, basi nikuongezee jambo la ziada KULALA ni hali ya roho kutoka ndani ya mwili na kuanza kuushangaa ama mwili wenyewe au mazingira yaliyoizunguka au huamua tu kutembea tembea huku na kule na hapa ndipo watu huota ndoto za ajabu kama kukimbizwa au kutaka kutokewa na jambo fulani kisha ghafla huzinduka toka usingizini na kuhema juu juu. Hali hii huzitokea roho zinazozurula.

Labda utapata swali, vipi wanaolala na kutokuamka kabisa?, je hawa hwa wana KUFA, FARIKI au WANAAGA DUNIA? Hawa hawapo kwenye kundi lolote kati ya haya matatu. Kifupi ni kuwa hawa ni watu ambao wamepatwa na 'ajali tu' yaani hakukuwa na taarifa yoyote kati ya roho na mwili.

Huo ndio utofauti angu wa mambo haya matatu. Kumbuka utofauti wangu huu unaweza kuwa tofauti na mtazamo wako.

Je, unadhani ipo mifano ya kiimani itakayoweza weka mbolea kwenye dhana hii ya utofauti wa KUFA, KUFARIKI na KUAGA DUNIA? Basi usisite ongeza nyama nyama pia.



NIJUAVYO MIMI

KUFA NI GENERAL TERM YA KIUMBE CHOCHOTE KILICHO HAI KUAGA DUNIA, MMEA UNAKUFA, BINADAM ANAKUFA, NG'OMBE ANAKUFA, NDEGE ANAKUFA NK


KUFARIKI NI SPECIFIC ACT YA BINADAM PEKEE KUAGA DUNIA.... MMEA HAUFARIKI, ILA BINADAMU HUFARIKI, NG'OMBE HAFARIKI, HUFA, NDEGE HAFARIKI ILA HUFA, KWAHIYO KUFARIKI NI KWA BINADAM TUUU

NAWASILISHA
 
Hapana tatizo mkuu baadhi ni The four agreements by Don Ruiz, The Vortex kimeandikwa na Jerry Hicky na Esther, Invisible acts of power by Caroline, Bible na Quran pia mkuu huwa nazipitia pamoja ila kikubwa zaidi huwa nasoma sana articles na posts kwenye forum tofauti tofauti hasa za Quora.
Ahsante sana mkuu.
 
kuafiki sio kufa bali ni kutoka sehemu moja kwenda nyingine. mf umetoka Dar - Moro hapo we utakuwa umefariki ila ili ioneshe kuwa umekufa inabidi uongeze neno dunia ie amefariki dunia hapo itakuwa umetoka katika hali ya uzima(dunia) na kwenda katika hali ya ufu.
kufa ni kutokwa na uhai hiyo haina mjadala.
 
Back
Top Bottom