SoC02 Huu ni utumwa katika Elimu

SoC02 Huu ni utumwa katika Elimu

Stories of Change - 2022 Competition

Abdideol

Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
13
Reaction score
6
Huu ni Utumwa Katika Elimu.
Ni wazi kuwa hakuna umuhimu wa Elimu bure maana cha bure hakina Thamani.

Udogoni tumekimbia sana kukwepa kujisomea jioni na wazazi walituacha tu ila hatukujaribu kukwepa tuition tukihofia wazazi kutuadhibu yote sababu tunaonekana kuchezea pesa yake ambayo anaitoa kwa uchungu.

Leo hii tunaletewa Elimu Bure cha ajabu vijana wakiume kwa wakike wanaongezeka mtaani kwa kukwepa Elimu hiyo cha ajabu hakuna Mzazi wala Kiongozi wa mtaa kujishughulisha na wanafunzi hao, "Ata usipoenda shule sina hasara na wewe" Mzazi akiamini kuwa yeye hana hasara katika hilo.

Muathirika katika hili janga litokanalo na Elimu Bure ni Mtanzania wa kipato cha chini yaani Mjasiliamali mdogo asiyeweza kumpeleka Mtoto huko katika mashule yenye hadhi ya juu na yanayoongoza kwa ufaulu kila kukicha.

Hatukuwahi kusoma shule za kata sawa na watoto wa wabunge/ Mawaziri au viongozi wengine.

Leo unakuja kuona kiasi gani tunaandaliwa kuwa Watawaliwa {Watumwa} ndani ya shule zetu za Serikali lakini Watoto wao wanaandaliwa kuwa {Watawala/washikamamlaka} Nje Ya Shule za Serikali.

Huu utumwa tunaendelea kuufurahia kwa kukosa maarifa. Tathimini

Nitambue kwa jina
ABDIDEOL RUHETTAH
 
Upvote 0
Back
Top Bottom