Zanzibar 2020 Huu sasa ni ufalme; haiwezekani watoto na familia ya Mwinyi iteuliwe kugombea kuanzia Urais hadi Ubunge

Zanzibar 2020 Huu sasa ni ufalme; haiwezekani watoto na familia ya Mwinyi iteuliwe kugombea kuanzia Urais hadi Ubunge

Hata Mizengo Pinda nimeona jina la mwanae limepita simiyu huko...... Hatari sana
 
Then Kuna the kijazi's..... CCM akili zao wanazijua wenyewe
 
Kwanza nawapongeza wajumbe kwa mamuzi yenu mazuri ya kuwachinja wagombea waliokimbilia CCM ili wawaangushe wazawa wa CCM
swali langu dogo kwanini watoto wa Baba wa Taifa hakuna hata mmoja mliyempitisha?

Kwanini watoto wa mwinyo wamepewa fursa kubwa ya Urais na Ubunge?

Je, hii inaashiria nini kwa familia ya Baba wa Taifa?

Si ashakufa , CCM unawajua wewe!!!!!
Hata Mwinyi akifa atafanyiwa vivyo hivyo
 
Sioni kama ina madhara yoyote iwapo nia na uwezo wanao. Nimekumbuka hii ilishawahi kutokea kwa upinzani enzi za mzee wetu Philemon Ndesamburo (RIP) kazi zikaendelea tena vizuri tu
Kikubwa wawe na uwezo
 
#Ufalme au?

Hussein Ali Hassan Mwinyi ~ Mgombea URais Zanzibar

Abbas Ali Hassan Mwinyi-
Ubunge ~ Fuoni

Abdalla Ali Hassan Mwinyi -
Mbunge ~ Mahonda

Zubeida Shaibu (Mkewe Abbas Ali Hussein Mwinyi)
Mbunge ~ Mfenesini
Umechukua forms za kugombea ukanyimwa? Hao wamechukua forms mkuu na wakaendelea na utaratibu mpaka hapo walupofika.

Wewe kama umechukua forms na ukanyimwa lete udhahidi hapa tujue tukusaidie vipi.

Binadamu wote hatuwezi kuwa sawa, tujaribu kutumia vizuri sehemu ambazo Mwenyezi Mungu katupa baraka kwenye kujiendeleza maisha yetu.
 
Kila mtu ana haki kikatiba, ila mama Kikwete na Mwinyi walichofanya sio sahihi. Mama salma kikwete angeachia hata ukoo mwingine nao ule national cake ya ubunge huko kwao kusini, maana yeye na mumewe wana asilimia 70 ya mshahara wa urais mpaka kufa kwao.
Kumbe hujui,2025 ni zamu ya muislamu so huyo mama anaandaliwa na Tiss kua mgombea na serikali ijayo atapewa cheo kikubwa ili kumjenga apate uzoefu,na hii itakua tu Kama hillar Clinton
 
Hivi hawawezi kumpa Pasco Mayala hata nafasi moja?

Wamwogope mungu
 
Mwenye nacho ataongezewa, asiekua nacho, hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa
 
#Ufalme au?

Hussein Ali Hassan Mwinyi ~ Mgombea URais Zanzibar

Abbas Ali Hassan Mwinyi-
Ubunge ~ Fuoni

Abdalla Ali Hassan Mwinyi -
Mbunge ~ Mahonda

Zubeida Shaibu (Mkewe Abbas Ali Hussein Mwinyi)
Mbunge ~ Mfenesini
Wanaangushwa na Maalim Seif Sharrif Hamad!
 
3/50 x100=6%
Asilimia 6 ya wabunge toka Zenji wanatoka nyumba moja!!!
Kama wakipita ubunge,na ndugu akapita urais,basi Baraza la Mawaziri la Zenji laweza kuwa 2/15 × 100 = 13.3% kutoka nyumba moja. (Hapa ni kama baraza ni mawaziri 15 na wawili wa nyumba moja wakawa mawaziri)
 
Saana tu
Uk kulikua na David milliband na Eddie Milliband,mmoja waziri wa Mambo ya nje,mwingine kiongozi wa wabunge
Us kulikua na Jeb na George Bush,bill na Hillary Clinton ndio demokrasia ukiona unapata kiungulia usiwape kura tu utapona fasta
Kwa hili mnatolea mfano mabeberu!!?
Mkiambiwa Demokrasia,haki na uwazi,mnasema hao ni wao na sisi ni sisi!!?
Leo beberu,kesho mnalala naye kitanda kimoja!!.
Kweli Mungu akikunyima akili, busara, werevu na maarifa,basi anakuwa kakuacha uchi.
 
Back
Top Bottom