Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kutokana na umri wangu wa kukaribia kuwa mzee, nimeamua kuwa bize na mambo ya Mungu, pamoja na kutofanya matumizi yasiyokuwa na tija.
Changamoto inakuja kwa michepuko yangu miwili; mmoja ana mtoto, mwingine ndio yuko mjamzito, atazaliwa huko baadaye.
Huyu mwenye mtoto; mara kwa mara ananisumbua anataka aje, alambe asali, kwa mtazamo wake kwamba hawezi kutoka na mwingine kwa kuhofia magonjwa; ila sasa, nikimwambia njoo; anasema anataka nimtumie nauli ya kuja na kuondoka, wakati uwezo wa kuwa na nauli anao.
Huyu mjamzito; ndio amezidi kabisa, ananiongelesha maneno ya kumtoa nyoka pangoni, mpaka nafikiria sijui nitoe akiba yangu yote ili aje alambe asali muda huu au vipi. Ingawa nikimwambia atumie salio lake, hataki.
Huu si ni utapeli ndugu zangu?