Kuna kundi kubwa sana watu hawajui kwanini WANAFUNGA, ila kwakuwa umefika mwezi wa Kufunga basi wanafunga tu kufata Mkumbo
Waliowengi wanafunga Kula, mtu aliefunga Kula hawezi kuvumilia kukuona wewe unakula kisha akaendelea kuact Normal mbele yako
Ndomana kuna sehemu watu wakionekana wanakula wanapigwa/kuchapwa fimbo,kufokewa,kudhihakiwa na mambo mengine ambayo sio ya kistaarabu
Nadhani viongozi wetu wa Dini zetu wangewekeza nguvu kubwa kwenye kuelimisha watu kwanini wanatakiwa Kufunga
Tofauti na hapo tutakuwa na kundi kubwa la watu wanaoshinda na Njaa ila sio kundi kubwa la wafungaji