Huu udini sasa hadi kwenye biashara?

Umemalizaaaa
 
Wabongo acheni ushamba mtu anaefanya biashara inamaana ana uhuru wake na anahaki yakutotoa huduma kwa sababu zake iyo ndo financial freedom
Mtu amefunga kwa imani yake wewe unakuja kulalamika uku jf unataka kulazimisha mtu akuuzie chakula wakati amefunga kwani wauza vyakula wote ni waislam

Hizi hoja za chuki chuki nashindwaga kuzielewa mbona watalibani wanavumilia siku zenu za ibada mkifunga biashara waacheni na wao wamalize ibada yao mbona huduma unaweza pata sehemu nyingi tu fungeni milango ya chuki iyo muishi kwa amani
 
Hata ukiagiza maji/soda kwenye duka la mpemba wanakuambia hawauzi.
 
Umeona eeh? Kwamba mimi sili na wewe usile. Siyo kwamba anafunga kwa ibada ya roho yake. Mbona Hyatt hotel ni ya muarabu na serena hotel ni ya mpakistani ila msosi upo mda wote na futari ipo jioni pia. I'm sure ukienda Dubai mchana huu hukosu msosi.
Dubai Airport msimu wa sikukuu ya Christmas hupamba kwa miti ya Christmas.
 
Waimani zingine mna kwarezma
 
Sasa mtu kama baresa anafunga migahawa yake kwanini? Wakati wafanyakazi wake wengine ni wakristu? Au anaajiri kidini?

Kwa mtu mdogo kama mama ntilie ambaye anapika mwenyewe naweza kukubali afunge ila kampuni kubwa kama baresa inafunga migahawa yake kisa mmiliki kafunga? Kumbuka hii ni kampuni kubwa. Mbona Serena ni ya mpakistani na hyatt ni ya muarabu wote waislamu ila msosi upo mda wote pale.
Alafu kama kufunga migawahawa ndo atapata thawabu kwa mungu basi basi afunge na kiwanda ambacho gari zinapakia unga wa ngano, sembe mda wote si hadi wakristo wananunua na kwenda kula mchana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…