Huu ugonjwa tusiuletee macheko

Huu ugonjwa tusiuletee macheko

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,589
Reaction score
35,268
Binafsi nilishangaa Sana kusikia Katibu Mkuu Kiongozi, na Makamu wa Rais Zanzibar wamefariki kwa changamoto ya upumuaji (Korona in advance) viongozi wa juu kabisa wa kiserikali.

Nilishangaa pia jinsi misiba ilivyoendeshwa bila tahadhari yyte. Kwa uchungu nilihoji pia usalama wa Rais, kama walio karbu na Rais wanakufa Kwa huu ugonjwa basi Kwa vyovyote vile Raisi hayupo salama na nikasema itakuwa aibu ya karne kwa Raisi kufa kwa ugonjwa huo, sababu niliona kama tunaufanyia mzaha.

Bahati mbaya Jambo hili limejitokeza, so sad Kwa kweli na ni aibu, Dunia yote inapambana angalau kuweka mikakati madhubuti ya kujikinga, hata nchi zinazopinga chanjo ya Korona zimejiwekea utaratibu maalum wa kujikinga na mamlaka husika zinausimamia.

Sisi tunapinga chanjo lakin hatuna utaratibu wala mikakati madhubuti ya kujikinga, ni hatari sana hii. Mungu yupo, lakni kamwe Maombi hayakuwekwa kuwa mahali pa wajibu. Mungu hawezi laumiwa kwa uzembe wa mhusika. Kifo cha Rais kinaweza kikafanya tukajisahau tena lakini viongozi wengi wataendelea kushuka kaburini kama hli halitafanyiwa kazi.

Ifikie hatua hata viongozi mjithamini pia, na niseme Tu wazi, mamlaka za juu pamoja na wizara ya Afya kaeni haraka kuangalia namna ya kuipeleka nchi Kati Kati ya janga hili, inawezekana ikawa too late lakn bado kuna nafasi ya kufanya. Acheni mzaha kabisa, na bado viongozi wengi na wananchi hasa wazee ambao wapo relaxed, wapo hatarini na huu ugonjwa tukiendelea kuuchekea. Msiogope Hali ya uchumi wa nchi. majanga kama haya hubadirisha mkondo wa maisha hii ipo wazi watu watajishape tuu mbali na Gharama itakayojitokeza.

Nimalizie Kwa kusema viongozi wa juu wa hii nchi, tunaomba muiongoze nchi kwa utaratibu wa katiba na Sheria, muache kuiendesha nchi Kwa pressure ya mashambulizi ya matamko ya watu walioko nje akina Kigogo na wengine.

Ni aibu jaman kuutangazia uma ghafla kuwa Raisi amefariki, tena kwa ugonjwa ,whatever ni ugonjwa gani. Kwa nini hamkutangaza alipougua. Hata kusema tu kuwa amelazwa anaumwa ilitosha kabisa, hata kama mngechelewa kutangaza msiba wake watu wasingekuwa surprised. Mliwanyima haki wananchi; wenye kumuombea wangemuombea, badala yake mnasema Rais yupo salama anachapa kazi kweli? Makawakamata vijana wa watu waliopata taarifa ya kwamba Rais hayupo poa na kweli kumbe vijana walikuwa sahihi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa 🚶🚶🚶🚶
 
Kufa ni kufa babu. Hizo nyingine ni kuongeza complications na kuwapanikisha wananchi.

So far hakuna ushahidi kuwa kafa kwa UVIKO. Naomba nisieleweke vibaya, UVIKO upo ila sio kila anaekufa basi ndo umemuua unless kuna ushahidi unaoshikika.

Watu wasife kwa magonjwa mengine kwa kuwa kuna UVIKO??[emoji2369][emoji2369]
 
Nilipoona corona imeondoka na Maalim Seif, na hakuwa na muda mrefu katoka Chato kwa Magufuli, halafu kifo cha Balozi Kijazi (huyu sina uhakika kama naye pia alikuwa Chato), kisha tetesi za akina Lissu baada ya ukimya kutanda, moja kwa moja nikaunganisha dots.

Hakika kama ulivyosema mkuu, ni aibu sana kwa watu wenye akili. Tumekuwa taifa la kishamba sana. Binafsi wakati Samia Suluhu anatangaza TBC nilipatwa na msisimko mkali sana uliojazwa na mchanganyiko wa huzuni na aibu ya kunitosha.

R.I.P Rais Magufuli.
 
Ukiachilia mbali swala la msiba , mkuu ni aibu Sana aisee , mpak tunajishangaa , vyombo vya kimataifa vinavyoripoti kuhusu huu msiba daah , vinaongelea jambo moja tu , Raisi aliyepinga uwepo wa Korona afariki dunia
 
Kufa ni kufa babu. Hizo nyingine ni kuongeza complications na kuwapanikisha wananchi.

So far hakuna ushahidi kuwa kafa kwa UVIKO. Naomba nisieleweke vibaya, UVIKO upo ila sio kila anaekufa basi ndo umemuua unless kuna ushahidi unaoshikika.

Watu wasife kwa magonjwa mengine kwa kuwa kuna UVIKO??[emoji2369][emoji2369]
Uko sahihi kabisa. Uzee pia ni sababu ya kifo...

RIP mzee Magu..
 
Watuletee chanjo maisha yaendelee. Kama tunawaamini WHO kwa recommendations za chanjo za watoto chini ya miaka 5 kwanini na hii tusiwasikilize?
 
Huyu Mama aturudishe kwenye WHO guidelines halafu aagize chanjo na kuanza kuwachanja Wazee na wenye magonjwa ya kudumu
Tume kuwa wabishi imekula hadi Kichwa chonde chonde hali ni mbaya sana huku kitaa
 
Kufa ni kufa babu. Hizo nyingine ni kuongeza complications na kuwapanikisha wananchi.

So far hakuna ushahidi kuwa kafa kwa UVIKO. Naomba nisieleweke vibaya, UVIKO upo ila sio kila anaekufa basi ndo umemuua unless kuna ushahidi unaoshikika.

Watu wasife kwa magonjwa mengine kwa kuwa kuna UVIKO??[emoji2369][emoji2369]
Uvico ndo nini
 
Watuletee chanjo maisha yaendelee. Kama tunawaamini WHO kwa recommendations za chanjo za watoto chini ya miaka 5 kwanini na hii tusiwasikilize?

Aliyekuwa hataki chanjo kwa kiburi cha madaraka kaondoka. Sasa ni wakati wa taifa kurudi katika njia za kisayansi na sio kishirikina.
 
Back
Top Bottom