Huu ugonjwa unaitwaje?

BASHADA

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
513
Reaction score
148
Kuna rafiki yangu amekuwa na matatizo ya kifamilia alitofautiana na mke wake, mwisho wa siku mkewe akawa anataka watengane jamaa akawa anajaribu kila hali kusuluhisha. Japo tatizo lenyewe halikuwa kubwa madhara yake jamaa akawa anazimia na kupoteza fahamu mpaka akalazwa hospitali na mwishowe suluhu ikawa ni kumtafuta mke wake. Akimwona tuu jamaa anapona na mkewe wake akiondoka tuu hali inamrudia mpaka anadondoka na kushindwa kuongea. Huu ugonjwa unitwaje na dawa yake ni nini? maana mke hataki kurudi kwa jamaa. Njia mbadala ya kumponya jamaa ni nini?
 
huyu dodo kamfanyia mambo ya utamaduni .
 
huyu dodo kamfanyia mambo ya utamaduni .

acha hizo wewe...ni psychological diseases ambayo inaweza sana kutibika..bibi yangu anatatiz kama hilo asipomuona mwanae ambae ni mama yangu..
 
Dah,ugonjwa hatari sana huu.Mchongee kinyago kwa gharama zozote zile chenye sura ya mke wa jamaa,kiwepo ndani upande wa pili wa kioo na mkipe mavazi ya huyo mama.Wakati jitihada za usuluhishi zikiendelea kuepusha mauti,maana kila ugonjwa mwisho lazima uue.
 
ni mojawapo wa magonjwa ya akili, unaitwa panic attack. hutibiwa kwa njia iitwayo cognative behavioral therapy!!
 
mnhhhh...kama jukwaa hili linaruhusu na magonjwa ya kimila/kichawi kujadiliwa naomba ruhusa nijadili gonjwa hili na tiba yake...na akizidi kuchelewa amini nakuambia kiangazi hafiki huyooo...masika ikiisha tuuu june inaanza kiangazi.
 
hili si jukwaa la kujadili upuuzi. uchawi peleka kijijini kwenu huko.
 
Nashukuru anaendelea vizuri, tulichofanya ni kupeleka timu ya washauri (counseling). Acheni hayo mawazo ya black chemistry
 
Nashukuru anaendelea vizuri, tulichofanya ni kupeleka timu ya washauri (counseling). Acheni hayo mawazo ya black chemistry
Sasa wewe umeleta Thread watu wanakupa Ushauri wewe unawalaumu wasilete mambo ya black chemistry? Si ungemaliza hukohuko na huyo mgonjwa wako? Au ulitaka na wewe Watu wakujuwe kuwa umeleta thread yako hapa? Tafadhali usilaumu watu bure tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…