BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Kuna rafiki yangu amekuwa na matatizo ya kifamilia alitofautiana na mke wake, mwisho wa siku mkewe akawa anataka watengane jamaa akawa anajaribu kila hali kusuluhisha. Japo tatizo lenyewe halikuwa kubwa madhara yake jamaa akawa anazimia na kupoteza fahamu mpaka akalazwa hospitali na mwishowe suluhu ikawa ni kumtafuta mke wake. Akimwona tuu jamaa anapona na mkewe wake akiondoka tuu hali inamrudia mpaka anadondoka na kushindwa kuongea. Huu ugonjwa unitwaje na dawa yake ni nini? maana mke hataki kurudi kwa jamaa. Njia mbadala ya kumponya jamaa ni nini?