Habri JF kuna kitu naomba kukileta kwenu tusaidiane kulitatua. Tatizo la kutojiamini mbele za watu. Mtu anaweza akawa anajua kitu lakini akaogopa kujielezea mbele za watu.hasa linapokuja swala la kujielezea kwa english,tabia ya kuogopa kuchekwa utakapokosea kujielezea..ama inapotokea umesimama mbele ya watu nakuongea kwa kutetemeka sana. Ila linapokuja swala la one on one talk aibu inapungua. ...ili tatizo madoctor linapunguzwaje? Mtu afanye nini kujipa confidence ya kusimama mbele ya watu na kijielezea bila kuonyesha mtetemeko wa sauti kuashiria amejawa uwoga. Nawakilisha kwenu....