Leo asubuhi nimekutana na video mbili zinazosambaa sana mitandaoni ambazo kwa kweli zinahuzunisha na kusikitisha. Video hizo zinaonyesha vijana wawili wakipigwa vibaya kwenye miguu yao kwa kutumia mpini, hali inayoonekana kuwa ni mateso ya kikatili yasiyo na utu.
View attachment 3532233
Kwa sasa, haijulikani tukio hili limetokea wapi, wala ni mazingira gani yaliyopelekea vijana hawa kufanyiwa vitendo hivi. Wengine wanadhani huenda walikuwa wahalifu au wezi, lakini hata kama hilo lingekuwa kweli, hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria kiasi cha kujichukulia mamlaka ya kuadhibu kwa mateso. Haki inapaswa kutolewa kupitia vyombo halali, si kwa ukatili wa kujichukulia sheria mkononi.
Ninaomba kuuliza na kusisitiza yafuatayo kwa jamii na hususan kwa vyombo vya dola:
* Je, Jeshi la Polisi lina uwezo wa kutumia teknolojia za kisasa kama video geolocation na video geotagging kubaini eneo halisi ambako video hizi zilirekodiwa?
* Je, inawezekana kufungua jalada la uchunguzi (case) dhidi ya mtu au watu waliowapiga vijana hawa, hata kama wahanga hawajajitokeza bado?
* Ni hatua zipi raia wanapaswa kuchukua wanapokutana na ushahidi wa video unaoonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kama huu?
View attachment 3532234
Jamii inayokaa kimya mbele ya ukatili inajenga mazingira ya hatari kwa kila mtu. Leo ni wao, kesho inaweza kuwa mtu yeyote. Haki, utu na uhai wa binadamu lazima vilindwe bila kujali mazingira.
Natoa wito kwa mamlaka husika, wanaharakati wa haki za binadamu, wanasheria na wananchi wote wenye dhamira njema: tusifumbie macho vitendo vya kikatili vinapowekwa hadharani. Teknolojia ipo, ushahidi upo—kinachohitajika ni hatua.
Tafadhali, yeyote mwenye taarifa sahihi au uelewa wa kisheria juu ya namna ya kushughulikia suala kama hili, achangie hapa. Ukatili si haki kabsa. Kujichukulia sheria mkononi si suluhisho.
Nimeshapata masaibu ya kuibiwa, naelewa machungu ya kuibiwa ILA kama tunataka kuwa na jamii iliyostaarabika hii siyo sahihi.Kama ni wezi Hiyo ni haki yao
Nani aliepiga nyuklia Japan?Tofauti ya mzungu na muafrika siyo langi ni roho na maono yaliyopo ndani yao.
Unauliza au unajibu, hivyo vilikua ni vita vyenye malengo maalumu siyo vita vyenu hivi vya kubondana miguu kisa wizi, vita pekee yenye mantiki hapa bongo ni ya Nyerere kwenda kumng'oa bonge la dada wa uganda.Nani aliepiga nyuklia Japan?
kama mwizi auwawe kabisaLeo asubuhi nimekutana na video mbili zinazosambaa sana mitandaoni ambazo kwa kweli zinahuzunisha na kusikitisha. Video hizo zinaonyesha vijana wawili wakipigwa vibaya kwenye miguu yao kwa kutumia mpini, hali inayoonekana kuwa ni mateso ya kikatili yasiyo na utu.