SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Kwa kipindi kirefu sana, wananchi wa nchi pendwa ya kizalendo ya Tanzania walikuwa na malalamiko ambayo kwa sasa ni dhahiri inaonekana yamepata ufumbuzi kufuatia ukimya uliopo.
Yale malalamiko ya wananchi haswa kwa wabunge na madiwani wao yamepungua sana kiasi kwamba ni adimu kukutana na wananchi wakilalamikia kero hadharani kama ilivyokuwa awamu zilizopita kupitia vyombo vyetu pendwa vya habari nchini kama TBC, ITV na vingine..
Ila ajabu ni kwamba wabunge wetu safari hii tunawaona kila mara majimboni wakija tena kuulizia shida zetu zinazotusibu na hata wengine kwa upendo kugawa vifaa vya elimu kwa wanafunzi kama Madaftari n.k
Kuna baadhi ya wananchi wachache wanaobeza utendaji wa viongozi ambao wako mitandaoni kuchafua watendaji wetu mahiri walio kwenye majukumu yao kutimiza kile walichoahidi kabla ua Uchaguzi mtukufu wa October 2025..
Pongezi kwa serikali yetu sikivu katika kuhakikisha kuwa DIRA 2050 inafanyika kwa vitendo..
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Tanganyika. Mungu wabariki viongozi wetu wachapakazi.
NB:
Ukiona huelewi mshirikishe jirani yako.