Huu umeme wetu unakatika kama Angel Nyigu

Huu umeme wetu unakatika kama Angel Nyigu

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Naona finally kama yalivyokuwa matarajio yao, Watanzania tumenywea kama nini sijui. Tuko busy kujadili Harmonize kuachana na Kajala.

Na embu tuchukulie kweli hili tatizo liko nje ya uwezo wa serikali kulitatua, embu tuchukuliè tu ni kweli. Hivi kwa nini sijawahi kuona serikali ikihamasisha watu wapunguze matumizi kwa hiari katika kipindi hiki cha dharura kama hatua ya kwanza kukabiliana na tatizo? Kwa kuwa Watanzania ni waelewa sana na wasikivu, inawezekana hiyo kampeni ikafanikiwa na kupunguza makali ya mgao.

Pia serikalini na katika sekta zingine, wote wangehamasishwa kwanza kupunguza matumizi yao ya umeme kwa jinsi wawezavyo bila kuathiri sana shughuli zao. Kwa mfano, haileti mantiki leo hii tuko katikati ya changamoto hii bado kuna mechi za ligi zinachezwa usiku.

Huu umeme kwa kukatika huku kwa nini usijisajili tu BASATA ukaimba Singeli maana nikisema Amapiano itakuwa kama Mmasai kuingia disco.
 
Back
Top Bottom