Huu upepo si mzuri kwa Spika Tulia. Je, unaweza kupita naye?

Huu upepo si mzuri kwa Spika Tulia. Je, unaweza kupita naye?

Kuna mambo ukiyaangalia kwa undani sana Tena kwa jicho la tatu utagundua kuna kaupepo fulani kana mchanganyiko wa joto na baridi kakivuma upande wa kiti Cha Spika. Je, upepo huu una madhara kwake?

Mambo fulani fulani yanatoa picha ya vuguvugu la upepo huu. Kwanza, kitendo Cha Shabiby kusema kauli yenye kuashiria Jambo zito, nanukuu sehemu ya kauli yake "...hata wewe Spika ukileta siasa zako tutakuazimia". kwa wenye kuangalia mambo kwa jicho la tatu watagundua kauli hiyo imebeba kusudi na dhamira. Je, ni siasa zipi Spika anazifanya? Je, zipo kinyume na sera za CCM?

Jambo la pili, Punde tu baada ya kupokea ripoti ya CAG kamati kuu ilikaa na kutoa maazimio kwa Serikali kuchukua hatua za haraka kwa wote waliohusika na ubadhirifu. Spika ni mjumbe wa vikao vya kamati kuu na azimio hilo aliridhia. Kama mchakato wa kuchukua hatua ,unaanzia bungeni huku Spika amesema kwamba Ripoti itajadiliwa mwezi Novemba. Je, utekelezaji wa maazimio ya kamati kuu utakuwaje?

Jambo la tatu, wakati wa mjadala wa mambo ya ushoga , Spika aliagiza Serikali ifanye mabadiliko ya sheria. Kwa uelewa wangu mdogo, sioni kama spika ana mamlaka ya kuiagiza Serikali. Kwa sababu katika mchakato wa kubadili sheria , serikali hupeleka muswada bungeni na mwisho bunge huufanya muswada kuwa Sheria. Je, Spika ana hayo mamlaka?

Nne, kitendo cha Waziri Mkuu na Makamu wa Rais kwa nyakati tofauti wameweka mkazo wa kuchukua hatua kali kwa haraka kwa wahusika waliotajwa na ripoti ya CAG. Je, hiyo inaashiria nini?

Hapa ndipo akili ya ziada inatakiwa itumike katika kuona kilichopo katikati ya mstari. Nimalizie kwa kusema ,huu ni upepo mbaya sana kuelekea kwenye kiti Cha Spika. Je ,upepo utapita naye au utavuma na kutulia ?
Sioni dalili kuondolewa kwake Kwa Sasa ila anaweza ondolewa Kwa kuwaacha Chadema washinde Jimbo la Mbeya Mjini..

Licha ya kuaminiwa na Rais ila Bado ana akili za kimwendazake Mwendazake
 
KUMWONDOA SPIKA AU NAIBU SPIKA MADARAKANI

Taarifa ya Hoja ya kumwondoa Spika Madarakani 158.

(1) Mbunge yeyote anayetaka kuwasilisha hoja ya kumwondoa Spika madarakani chini ya Ibara ya 84(7) (d) ya Katiba, atawasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu akieleza sababu za kutaka kuleta hoja hiyo.

(2) Mara tu baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu ataipeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuijadili.

(3) Endapo Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaridhika kuwa zipo tuhuma mahsusi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya Ibara ya 84(7) (a), (b), (e), (f), (g) na (h) ya Katiba, Sheria au Kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi Kamati hiyo itaidhinisha kuwa hoja hiyo ipelekwe Bungeni ili iamuliwe.

(4) Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala.

(5) Spika atakuwa ameondolewa kwenye madaraka endapo zitapigwa kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya Wabunge wote za kuunga mkono hoja hiyo na uamuzi wa Bunge utafanywa kwa kuzingatia kura za siri.

(6) Spika anayetuhumiwa anaweza kujiuzulu nafasi yake kwa kutoa maelezo ya kujiuzulu kwake Bunge
Naomba mjadala huu ufungwe kwa comment hii.asante
 
Ila Tulia Ackson ni kichwa aise pamoja na yote. Sidhani kama aliongea hayo yote kwa kukurupuka. Naamini ni mtu msomi na anaijua nafasi yake. Ova
Kabadili gia angani na usomi wake. Ova
 
Nyie genge la wasukuma mtahangaika sana mpaka mjinyee hadharani hamtafanikiwa hata kwa nukta moja. wakati wa marehemu wenu ripoti za CAG ZILIWAHI KUJADILIWA? Mlikuwa wapi wakati ule? Nje ya nchi? Washamba msio na haya mliojaa ubinafsi. Hii nchi si yenu wenyewe hamjatosheka na upendeleo wote mliofanyiwa?
Mama mwenyewe ameonyesha kukasirishwa na ufisadi uliofanyika, hili ni suala la kupongezwa hata kama huko nyuma haikuwahi kujadiliwa huyu ni wakati mzuri kwa mustakabali wa nchi yetu
 
Ila Tulia Ackson ni kichwa aise pamoja na yote. Sidhani kama aliongea hayo yote kwa kukurupuka. Naamini ni mtu msomi na anaijua nafasi yake. Ova
Ni kilaza mkubwa! Sasa report ya CAG kijadiliwa baada ya bunge la bajeti.
 
Tusisahau Ni ugomvi wa kunguru kwa kunguru na utaamuliwa na kunguru mkuu.

Shambani kwa bibi kumenoga.
 
Nkisikiaga issues za CAG kama ni radio nazima.
We have never been serious na huu upigaji ever since.
Am sure at hii report itapita watachukuliwa wachache wa kutolewa kafara maisha yatasonga alafuu watu hao hao watapeta 2025
 
Hivi ni kwanini Katibu wa Bunge anateuliwa na Rais ambaye ni Mkuu wa Mwimili mwingine?
Rais ni Mkuu wa Nchi. Wewe unataka kumchukulia Rais kama Mkuu Serikali(executive) tu. Unasahau hicho cheo cha Mkuu wa Nchi. Mkuu wa Nchi ndio mwajiri mkuu.
Katibu wa Bunge ni Mtendaji. Lkn pia kama ana nafasi za kuteua wabunge, kwanini akose kumteua Katibu?
Isitoshe, mhimili mmoja kuwa stronger, strongest ni muhimu ili kuwa na breakthrough. Balance of power can cause a deadlock.
 
Sudan wamefikia walipo now kwa sababu ya pande mbili kukaribiana sana nguvu baada ya Omar Ole-Bashir kung'olewa.
 
Back
Top Bottom