Huu utamaduni wa vyombo vya habari kuhoji wafiwa sio mzuri

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Hii tasnia ya habari kwa sasa ni kama haina maadili kabisa.

Inakuwaje mtu yupo kwenye majonzi unamuhangaisha ili wewe upate views na likes za kukupa fedha?
Mazishi ni ibada ndugu zangu!
 
Ulikuwapa wapi kutoa ushauri huu wakati watu wanalazimishwa kwenda kuona mwili wa magu alipoondoka kuelekea jehanamu?
 
inakuwaje mtu yupo kwenye majonzi unamuhangaisha ili wewe upate views na likes za kukupa fedha?
Mazishi ni ibada ndugu zangu!
ni vizuri kuwahojiwa na wakatoa maelezo kuondoa taharuki na upotoshaji unaowezakua unasambaa mitandaoni dhidi ya kifo cha mpendwa wao 🐒
 
Ulikuwapa wapi kutoa ushauri huu wakati watu wanalazimishwa kwenda kuona mwili wa magu alipoondoka kuelekea jehanamu?
Uliona Mama Janet akihojiwa?
 
ni vizuri kuwahojiwa na wakatoa maelezo kuondoa taharuki na upotoshaji unaowezakua unasambaa mitandaoni dhidi ya kifo cha mpendwa wao 🐒
huo ni utamaduni wa wapi?
 
Tofautisha vyombo vya habari na wasaka viewers ,,hauwezi kuona Azam tv,Itv au Tbc wakafanya huo ujinga
 
huo ni utamaduni wa wapi?
ni utamaduni wa wafiwa kote ulimwenguni, kuelezea waombolezaji kinagaubaga mwanzo mpaka mwisho, ilikuaje mpaka marehemu akafikwa na umauti kuliko kila muombolezaji kujitungia tu sababu zake 🐒
 
Umeanza lini na umeanzia wapi?
 
Uliona Mama Janet akihojiwa?
Sikumfuatilia maana sikushinda kuangalia kila chombo cha habari, bali niliona ndugu na jamaa wa familia yake wakihojiwa. Au mama Janet pekee ndio aliyekuwa mfiwa kwenye msiba wa dhalimu?
 
Back
Top Bottom