Huu utaratibu mpya wa mazishi kipindi cha siku za karibuni unafikirisha

Huu utaratibu mpya wa mazishi kipindi cha siku za karibuni unafikirisha

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Moja kwa moja kwenye mada.

Tangia see seke la haka kaupepo liongeze kasi kumekuwa na mengi ya kufikirisha.

1. Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote lakini serikali imechagua kuweka siri utambulisho wa wanaopitiwa na haka kaupepo au hata kufa kutokana na kaupepo kenyewe.

Hii ni tofauti na nchi zingine ambako utambulisho wa watu ambao haka ka upepo kanawapitia au hata kufariki kumeweza kuwafanya watu kutambua vilivyo hatari iliyoko mbele yao na hivyo kujipanga kwa hatua na tahadhari muafaka zaidi.

Kwani kuugua au hata kufa kwa haka kaupepo ni jambo la aibu au la ajabu?

2. Mazishi ya watu maarufu bila kujali chanzo cha ugonjwa wamekuwa wakizikwa haraka haraka (bila kujali dini zao). Inaeleweka kuwa siku hizi waombolezaji wanakuwa wachache. Lakini hili la uharaka na kutofungua majeneza kwa heshima za mwisho kwetu sisi wakristo haya ni mageni.

Ama kwa hakika imekuwa ni taratibu mpya mpya bila kujali marehemu amefariki kwa ugonjwa gani. Yaonyesha uelekeo sasa ni kutoruhusu kumwona marehemu kwa mara ya mwisho na kumzika bila kusubiria (yaani chap chap).

3. Kingine ule utaratibu wetu wa kusafirisha au kusafirishwa. Alisema spika "tutajitahidi kweli huyu mwenzetu akazikwe kwao ..." Mwisho wa kumnukuu.

Inafikirisha sisi makapuku wengine je nani atajitahidi tukazikwe makwetu?

Yote haya yanaonekana kuwa ni athari tu za haka ka upepo. Sembuse mtu akifa kabisa au hata haka kaupepo kakamkumba?

Hili nalo lina fikirisha. Kimya kimya, kwa nini utaratibu huu mpya unatokea katika kipindi hiki?

Ana kweli Corona si kaupepo bali kama ni gonjwa, tena ni baba lao!

Hiiiii bagosha!
 
Je hao wakubwa wanaokufa kwa covid-19 na kusafirishwa mpaka makwao hawaenezi huu ugonjwa? Inakuwaje serikali ya wanyonge inawabagua wanyonge wake na kuwazika chap chap usiku kwa sesa? Tafadhali mjitafakali.
 
Je hao wakubwa wanaokufa kwa covid-19 na kusafirishwa mpaka makwao hawaenezi huu ugonjwa? Inakuwaje serikali ya wanyonge inawabagua wanyonge wake na kuwazika chap chap usiku kwa sesa? Tafadhali mjitafakali.

Mkuu yaweza kuwa hawa wakubwa hawajafa na covid-19. Labda ni utaratibu mpya tu wa mazishi. Nasema hivi kwa sababu wamekuwa wakisema taarifa kuhusu Corona ni wao tu na hawajatuambia kuna kigogo kafa na huo ugonjwa.
 
Back
Top Bottom