Huu utaratibu wa kupeana hela kama mihadarati upo mpaka kwenu huko?

Huu utaratibu wa kupeana hela kama mihadarati upo mpaka kwenu huko?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Katika tabia siipendi tuliyo nayo watanzania ni hii ya kuficha ficha mambo ambayo hata siyo ya kuficha

Mfano kwenye kazi ambazo zinafanywa na team...kazi mnaanza vizuri mnafanya vizuri linapokuja suala la kugawana posho utashangaa kiongozi wa msafara na mlipaji wanaenda kujificha sehemu eti kuteta yaani pesa za watu zinagawanywa kama bangi.

Watu mmeenda kulima wote au kujenga kwanini mlipaji asiweke wazi malipo ya kila mmoja au malipo ya kazi yote badala yake anamuamini mtu mmoja kwamba yeye ndo aje kuwagawia matokeo yake malalamiko hayaishi..

Kila mtu anafanya kazi hili taifa na anastahili posho hivyo mwenye kutoa haki atoe haki.

Vipi kwenu huko kwenye maokoto tajiri humlipa kila mtu kwenye account yake au ndo mambo ya kumkabithi mtu wa kati mzigo aje awagawie?
 
Back
Top Bottom