Huu utaratibu wa TBS utaumiza sana watu!!

Simbamteme

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
804
Reaction score
2,131
Nimeona tangazo la TBS(Nimeli attach hapo) kuwa kuanzia mwezi March mtu akiagiza gari kutoka nje,halitakaguliwa hukohuko nje

Utaratibu uliopo sasa ni kuwa gari inakaguliwa hukohuko nje kupitia kwa mawakala wa TBS(Ambao mm kwa maoni yangu naona ndo mzuri zaidi) kwani gari likikutwa lipo chini ya kiwango haliwezi kusafirishwa kuja huku...ni ama ubadilishiwe ama uwe refunded

Sasa kwa mujibu wa Tangazo lao ni kuwa kuanzia mwezi March,ukiagiza gari kutoka nje,HALITAKAGULIWA..litasafirishwa kuja nchini then TBS watalikagua..likikutwa lipo chini ya viwango,litapelekwa karakana kwa ajili ya matengenezo(hapa lazima hela ya matengenezo ikutoke na hii itakuwa ni nje ya hela ya ukaguzi)...Hapo bado TRA wanakusibiri wakamue hela yako

Sasa najiuliza..itakuwaje kama ukikuta gari inahitaji matengenezo yatakayohitaji hela nyingi sana?hii si itakuwa chanzo cha watu kukimbia magari yao?

TBS inabidi iangalie hili swala kwa jicho pevu...Nchi itageuka kuwa DAMPO la magari yasiyo na viwango

Na kwa mtazamo wangu nahisi hii yote ni kwa sababu ya kutaka kukwepa kugawana hela na Mawakala wao waliopo nje

Mnaotarajia kuagiza magari kuanzia mwezi March mjiandae..Ukiagiza gari "mkweche" ujue ishakula kwako hiyo

 
nimetoka juzi pale NIT kuipeleka ist kukagulkwa ili ipite na tbs kwa ajilli ya ukaguzi bwana kama una roho nyepesi unaweza mpga mtu ngumi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],kuna masai amepeleka kapaso kake 4 piston akajiona kanunua chases no katakuwa kazima bwana bwana kwenye kutestiwa kamepigwa speed mpka 160km/hr.dah kigari mpka kikazima chenyewe akaambiwa akiweke pembeni wakati huo masai jicho jekunduuu
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sasa hayo matengenezo na ukaguzi vinawahusu nini lakini mbwa hawa?!

Kwanza wamekubaliana na nani kuhusu huo utaratibu usioeleweka?!

Kama system ya kwanza haikuwa na shida kwann wanaibadilisha sasa?! Mbona wamekalia upumbavu hawa watu lakini....?!
 
Sasa hayo matengenezo na ukaguzi vinawahusu nini lakini mbwa hawa?!

Kwanza wamekubaliana na nani kuhusu huo utaratibu usioeleweka?!

Kama system ya kwanza haikuwa na shida kwann wanaibadilisha sasa?! Mbona wamekalia upumbavu hawa watu lakini....?!
Mitano Tena
 
Mngewachapa ata vibao vya bahat mbaya
 
Wanatengeneza mazingira ya Rushwa.

Hao ndio wabongo chini ya meko jitu
 
Hakuna wa kumlaumu, watu walimkataa Jiwe akaiba kura. Tusilaumane labda tulaumiane kwa kutopinga matokeo kwa kuingia barabarani!
Wewe uliingia barabarani?ulitaka uingie na nanii kupinga matokeo?
Rafiki yangu achana na ushabiki utazimia siku moja fanya yako usiwashirikishe watu.

Kama kweli ulikuwwa na nia ya kuingia barabarani hata sasa unawezaingia wewe na ukoo wako,saw?
 
Hahaha. Aisee.
 
Wewe uliingia barabarani?ulitaka uingie na nanii kupinga matokeo?
Rafiki yangu achana na ushabiki utazimia siku moja fanya yako usiwashirikishe watu.

Kama kweli ulikuwwa na nia ya kuingia barabarani hata sasa unawezaingia wewe na ukoo wako,saw?
usitake niwe kama wewe. tunatofautiana.
 
Hawa jamaa watazidiwa na kazi kitu ambacho kitapelekea rushwa kubwa sana na naona hata watu wakiambiwa walipie storage wakati wanasubiri gari ifanyiwe inspection

Tusubiri tuone
 
Hii serikali sijui huwa inafikiria kwa kutumia nini..!

Yote uroho tu wa kodi ,,,nchi inapelekwa mpaka miaka 20 nyuma iwe kumiliki gari ni anasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…