Wewe hujaelewa!!hata sasa utaratibu uliopo ni kuwa unanunua gari, kisha kabla ya kulisafirisha kuja nchini, kuna mawakala wa kulikagua ambao wameidhinishwa na TBS, kama litashindwa kutimiza vigezo, litarudishwa kwa muuzaji, na utapewa gari lingine, ndio linatumwa kuingia nchini!!shida ya utaratibu huu mpya ni kuwa , mtu una safirisha gari hadi nchi, unafika huku unaambiwa halijatimiza vigezo!!!lazima ulitengeneze kwa gharama zako, tena sio gereji za mtaani, ni kwenye za serikali!!hapo kifupi limetengenezwa chaka tu la kupatia pesa!!ila kama ni gari ambalo limeshaingia nchini ukilinunua kwa mtu haina haja tena ya TBS, kulikagua.