Huu utaratibu wa TRA kufanya kazi ukoje?

Huu utaratibu wa TRA kufanya kazi ukoje?

Oppomall

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
3,683
Reaction score
3,966
Habari za wakati huu wakuu?
Nimeshangazwa kidogo na jambo nililolishuhudia leo kutoka kwa hawa watendaji wa TRA,nimeamua kuja hapa ili niweze kupata ufafanuzi ikiwa ni sahihi ama laa!
Hawa jamaa leo walipita maeneo ya mtaani kwangu leo wakifuatilia kodi kwenye biashara za watu mbalimbali kama maduka, vibanda hata magenge. Kinachonishangaza ni pale walipokua wanafika kwenye maduka ya watu ambao hawakutimiza masharti ya ulipaji kodi walikua hawafungi milango ya maduka yao kama ilivyozoeleka badala yake wakawa wanaondoka na bidhaa zilizomo ndani ya eneo husika na kumwacha mwenye Ofisi na mbao tupu. Huu nao ni utaratibu mpya au nimechelewa tu kuushuhudia?
Asanteni!!!
 
Hawa jamaa ni tatizo kubwa sana kwa wajasiriamali na wapiganaji wanaotaka kujikomboa kwa Taifa maskini kama Tanzania. Serikali haina budi kuangalia utendaji wao kama kweli wana nia ya kuliondoa taifa hili katika umaskini
 
Back
Top Bottom