Huu utata katika katiba pendekezwa

Endelea kupitia vifungu vyote ndugu ila mwisho wa siku jibu utapata kuwa katiba yote ni batili na instahili kupigiwa kura ya NO
 
Endelea kupitia vifungu vyote ndugu ila mwisho wa siku jibu utapata kuwa katiba yote ni batili na instahili kupigiwa kura ya NO

Moyo wa kuisoma Katiba Inayopendekezwa ni wa kiungwana, uhuru wa mtu kupiga kura ya ndiyo au hapana sii jukumu la kumlaghai mtu mwingine na kumhadaa afuate mawazo yako. Wewe mhimize mtu asome hiyo Katiba then yeye atumie uhuru wake muda utakapofika wa kufanya hivyo.
 
saf sana endelea kujisomea utagundua jambo kuhusiana na hii katiba pendekezwa na kisha uipigie kura ya kuipitisha,ila umenifurahisha kwa kuwa specific,kura ya ndiyo kwa katiba pendekezwa
 
saf sana endelea kujisomea utagundua jambo kuhusiana na hii katiba pendekezwa na kisha uipigie kura ya kuipitisha,ila umenifurahisha kwa kuwa specific,kura ya ndiyo kwa katiba pendekezwa

Nimeisoma na bado naendelea kuisoma yapo mapungufu ambayo sio lazima kuomba msaada wa kuelewesha hata kwa akili ya kawaida yanaonekana.

Kuhusu kupigia kura ni maamuzi ya mtu binafsi kuamua hapana au ndiyo bila kuangalia matakwa ya mtu au mrengo wa mtu
 
So what? Piga kura ya YESSSSSSSSSS
 
Kijana hapo umejichanganya we mwenyewe, soma vizuri uelewe hivo vipengele. Hakuna utata wowote hapo.

Utata upo tena siyo mdogo. Hasa pale hao makam wakitaka kuondolewa au wanapashindwa majukum yao. Yule Makam ambae ni Rais wa Zanzibar, akishindwa kaz ya Umakam, lakini kule Zanzibar aki-lideliver, haijafafanua itakuwaje. Hao wengine iko clearly stated!
 

unaongelea hii KATIBA PENDEKA iliyoletwa na FISADI CHENGE auuuu ipiii??
 

kama unaongelea hii KATIBA PENDEKA jibu lake ni HAPANA
 

Hakuna utata. Katiba inasema rais wa SASA wa Zanzibar anaweza KUPENDEKEZWA awe makamu wa kwanza wa serkali ya jmt IJAYO. By then (kama watashinda) atakuwa si rais wa Zanzibar tena, nao watakuwana Rais MPYA. WM
 
Hakuna utata. Katiba inasema rais wa SASA wa Zanzibar anaweza KUPENDEKEZWA awe makamu wa kwanza wa serkali ya jmt IJAYO. By then (kama watashinda) atakuwa si rais wa Zanzibar tena, nao watakuwana Rais MPYA. WM
Sawa sawa mkuu maana huyo dogo hapo juu hajasoma vizuri kakurupuka tu kutoa hoja ambayo majibu yake yanahitaji mtu asome kwa makini na kuelewa.
 
Hakuna cha NO au HAPANA, Ni KUSUSIA kabisa. Nitaeleza kidogo:

Kwanza: Katiba pendekezwa inatakiwa kususiwa maana mchakato wake ni batili tangu ilipoingizwa kwenye Bunge la Katiba. Katiba pendekezwa haina uhalali maana kura za Wabunge (Bunge la katiba) zilichakachuliwa ili kuipitisha.

Pili: Kura zote za NO zitabadilika na kuwa NDIYO endapo watu watajitokeza kupiga za NO maana Serikali wanataka kuipitisha' inyeshe mvua lije jua' na hakuna wa kuzilinda kura za HAPANA.

Suluhisho ni kuanza UPYA Bunge la katiba na mchakato ufanyike kwa maridhiano na kuheshimu maoni ya wananchi. Sula la kura ya maoni lifanyike kama procedure za kisheria tu lakn baada ya maridhiano ya kitaifa. Katiba inatakiwa ituunganishe WaTZ na sio kututenganisha na kuiacha nchi katika mpasuko

Ni uchungu sana na mateso kutii KATIBA ambayo hujairidhia na ambayo mchakato wake unalalamikiwa na makundi mengi katika jamii. Itakuwa ni katiba inayohamasisha ukiukwaji wa haki na sheria. Haitaheshimiwa kamwe.

Ngilenengo1




 

Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kususia kilicho chake na kutamani upotoshaji wa watu wachache kwa maslashi yao binafsi ambayo wanayaelewa wao wenyewe. Tuache kuwahadaa Watanzania na tumia maneno ambayo yatujenga Watanzania wote. Sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Hivyo wenye macho ya husda washindwe na walegee kwani wao wapo kwa manufaaa yao binafsi na matumbo yao wasiwahadae Watanzania.
 
Kila mtanzania analo jukumu la kuisoma katiba inayopendekezwa ili hatimaye afanye uamuzi sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…