Mmanu
JF-Expert Member
- Feb 11, 2015
- 1,775
- 1,011
Wakuu wa JF
Katika kupitia katiba pendekezwa nimekumbana na huu utata hususani katika sehemu ya Makamu wa rais
Ibara ya 99- inasema kutakuwa na Makamu wa rais watatu ambao ni
(a) Makamu wa kwanza wa rais
(b) Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa makamu wa pili wa rais na
(c) Waziri mkuu ambaye atakuwa makamu wa tatu wa rais.
Utata ukaanzia hapa:
Ibara 100(3) inasema Chama cha siasa chochote au mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi ya madaraka ya Rais, akiwa mgombea huru, hatazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea nafasi ya madaraka ya MAKAMU WA KWANZA WA RAIS kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika nafasi ya madaraka ya RAIS WA ZANZIBAR
Swali:
1: Je kama huyu rais wa Zanzibar atateuliwa kugombea nafasi ya makamu wa rais wa kwanza wa JMT hii nafasi ya umakamu wa pili wa rais bado itakuwa ni yake ama itakuwaje hapo?
2: Ikiwa yeye ndiye makamu wa kwanza wa rais wa Jamhuri ya Muungano na rais wa JMT akiwa hayupo katika nafasi hyo kwa muda mfano akiwa amesafiri je panapohitajika uwakilishi wa sehemu zote mbili yaani Tanzania bara na visiwani na ikiwa shughuli hyo inaulazima wa kuhudhuliwa na viongozi wakubwa sana katika pande hizi mbili?
3: Napatwa na kigugumizi namna ya utekelezaji wa majukumu kwa pande mbili yaani huku akiwa makamu wa rais na huku ni rais je majukumu yake atatekelezaje kwa wakati mmoja?
Naomba kufanunuliwa hapo ili nipate uelewa zaidi maana naona kama kuna double standard katika hyo nafasi.
Nawasilisha.