Lookmalasin
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,723
- 2,358
Yap inferiority complex imewajaa waafrika. Angalia mfano mdogo JF names na avatar zao. Wengi wanajiita majina ya kizungu na ya kiarabu wanaweka avatar za wazungu.1. Dini zimesababisha waafrika tunajidharau kwa kila hali. Tazama michango inayotolewa na baadhi yetu huku. Kile kiitwacho 'inferiority complex kinajidhihirisha'.
2. Leo hii mmakonde mkristu anashindwa kumuoa mmakonde muislamu kisa wazungu na waarabu walisema.
3. Majina ya kiafrika yanapotea. Ya kizungu na kiarabu ndiyo yanatawala. Utumwa wa kitamaduni.
4. Waafrika wamejazwa hofu ya mungu. Usipokuwa na hofu unaonekana wa ajabu. Hofu imefanywa kama 'value' fulani ya maana sana.
Hiyo inaonyesha inferiority complex yao vichwani yao na jinsi wanavyofikiri. Wanatukuza, kukuza na Kueneza utamaduni wa wageni. Wajapan, Wachina, Korea hawafanyi hivi.