Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Biashara ina upepo kama ajira tu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Mkuu hivi ukiwa unapiga biashara halafu mtaji ukakata na huna asset yoyote ya kuuza wala kukopesheka mtaji unautoa wapi?

Kuna wakati natamani niajiriwe ili ajira iwe backup ya mtaji maana kwenye biashara mtaji ni changamoto sana aisee
 
Mkuu hakuna mtu anamuibia mwajiri muda,tuna haki ya muda wetu wa ziada,Nadhani unachanganya biashara na uwekezaji,mpaka sasa Biashara inaonekana ni mwiba mchungu kwetu,mawazo tunahitaji hapa ni ya uwekezaji.
Uwekezaji unahitaji muda wako sana kama unataka kuona matokeo mazuri,kama utamtumikia mwajiri wako masaa8 bila kumuibia mda na wakati huo kunamtu umemweka kwenye biashara yako akusimamie tegemea maumivu lazma upigwe pa kubwa
 
Biashara ya Bar ni miongoni mwa biashara zenye return kubwa sana ila inataka uwe na strategist mzuri ili uendelee kubaki relevant sokoni, vinginevyo raia wanakuhama within few months.
 
Madini haya
 
Wakati huo pia utambue siku wenye nguvu wakija ni kuswaga mifugo Yako yote wanatia kwenye gari, kulingana na asili ya huko maana wizi wa mifugo ni nje nje tu.
 
Wakati huo pia utambue siku wenye nguvu wakija ni kuswaga mifugo Yako yote wanatia kwenye gari, kulingana na asili ya huko maana wizi wa mifugo ni nje nje tu.
naelewa boss, ishu ya usalama kwenye ufugaji ni changamoto sana.
 
Unaendesha hiyo biashara yako Kwa mtaji wa shilling ngapi?
Na Kwa mwezi unapata shi. Ngapi kama faida ukitoa gharama za uendeshaji biashara yako
 
UTT ni nzuri sana,binafsi nilishawahi kuweka mpaka nikafika 20m niliitoa nikafanyia jambo fulani,changamoto ya UTT return sio kubwa saana lakini pia si haba.
Mimi nimefikisha 70m nimeitoa mwezi uliopita. Ila nitaendelea tena. Ni sehemu ya kuhifadhi fedha huku ukiendelea kudunduliza ila siyo sehemu ya kutegemea faida kubwa.
 
Biashara nimeshajaribu tatu na zote zilinishinda,ni hela nilipoteza. Kwenye viwanja nakubaliana na wewe,lakini kwenye majengo nadhani ni mada fikirishi bado..Unaweka milion 60 yako kwenye nyumba,je ni lini utaona faida ya hiyo hela ulowekeza?
Sio kila mtu anaweza biashara kama umejaribu biashara tatu na zinabuma. Biashara is not your thing.
 
Pesa uliyowekeza NI shilling ngapi?
 
Good
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…