Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Biashara ina upepo kama ajira tu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Mkuu hivi ukiwa unapiga biashara halafu mtaji ukakata na huna asset yoyote ya kuuza wala kukopesheka mtaji unautoa wapi?

Kuna wakati natamani niajiriwe ili ajira iwe backup ya mtaji maana kwenye biashara mtaji ni changamoto sana aisee
 
Mkuu hakuna mtu anamuibia mwajiri muda,tuna haki ya muda wetu wa ziada,Nadhani unachanganya biashara na uwekezaji,mpaka sasa Biashara inaonekana ni mwiba mchungu kwetu,mawazo tunahitaji hapa ni ya uwekezaji.
Uwekezaji unahitaji muda wako sana kama unataka kuona matokeo mazuri,kama utamtumikia mwajiri wako masaa8 bila kumuibia mda na wakati huo kunamtu umemweka kwenye biashara yako akusimamie tegemea maumivu lazma upigwe pa kubwa
 
Kuna nyumba nilipewa nikarabati halafu nichukue kodi.
Ukarabati ulichukua Mil 8.
Ilinichukua miaka mi 3 kurudisha mil 8 kamili bila faida hata..!!!

Wakati huohuo nikafungua biashara ya Bar kwa mtaji wa mil 6 (nilishaifunga) ila mpaka inafungwa nilikuwa nimekusanya mil 15 (baada ya kutoa gharama zotee jumlisha kuhonga maaskari na maafisa wa serikali kama bwana afya) na kuiuza (kuifunga) kwa mil 6.7 kwa miaka miwili 2..!!!

Rudia tena statement yako???

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Biashara ya Bar ni miongoni mwa biashara zenye return kubwa sana ila inataka uwe na strategist mzuri ili uendelee kubaki relevant sokoni, vinginevyo raia wanakuhama within few months.
 
Guest lodge ni rahisi kusimamia kupitia technology unafunga CCTV camera kujua wangapi wamelala au unafunga sensor kwa bed inakaunti time ya mtu kalala masaa mangapi so kama kitanda hajijaguswa utajua.
Camera ufungwa kwenye corido.
Air b an b ni nyumba mfano wa Uber au bolt unaziweka mtandaoni pana watu au wageni wanakodi chumba kwa siku so inakuwa inaonekana dunia nzima unatoza kwa siku labda sh elf 8 au kumi so inategemea na mgeni anataka kukaa kwa siku ngapi.
Chumba self unajenga mtindo wa cotas, ujenzi wowote unarejesha hela baada ya miaka kumi,jengo ni kutunza pesa na pia ni mtaji siku ukipata mda umestaafu au kazi imeisha unaikopea then unafanya biashara unayoweza kusimamia mwenyewe tofauti na kuwapa watu wasimamie wengine wameandikiwa kuwa umasikini watazika pesa yako utaishia kulipa madeni bure ya mikopo.
Madini haya
 
Wakati huo pia utambue siku wenye nguvu wakija ni kuswaga mifugo Yako yote wanatia kwenye gari, kulingana na asili ya huko maana wizi wa mifugo ni nje nje tu.
Hii ishu ya ufugaji niliwaza kuifanya kwa large scale,Nitafute eneo kubwa huku mkoani Mara,nijenge mazizi na kijumba cha mchungaji,alafu niweke ng´ombe,mbuzi na kondoo. Ila ishu ya usalama wa hiyo mifugo ndio ilinipa wasiwasi maana inabidi ufuge eneo ambalo halina watu wengi,porini huko kwenye majani mengi.
 
Wakati huo pia utambue siku wenye nguvu wakija ni kuswaga mifugo Yako yote wanatia kwenye gari, kulingana na asili ya huko maana wizi wa mifugo ni nje nje tu.
naelewa boss, ishu ya usalama kwenye ufugaji ni changamoto sana.
 
Mimi ni mtumishi pia
Nina biashara 4, moja wapo ni Gas na uwakala wa fedha.

Mbona naona mambo yanaenda japo mtaji ndio changamoto??

Maana nahitaji biashara ziwe kubwaa ili niachane na ajira niwe 24 hrs enterpreneur, sasa mtaji banaaa CHANGAMOTOOO

Sijui niibe kama mafisadi mil 200 papp halafu unapita hivi...!!!

Mtaji changamoto aiseee.

#YNWA
Unaendesha hiyo biashara yako Kwa mtaji wa shilling ngapi?
Na Kwa mwezi unapata shi. Ngapi kama faida ukitoa gharama za uendeshaji biashara yako
 
UTT ni nzuri sana,binafsi nilishawahi kuweka mpaka nikafika 20m niliitoa nikafanyia jambo fulani,changamoto ya UTT return sio kubwa saana lakini pia si haba.
Mimi nimefikisha 70m nimeitoa mwezi uliopita. Ila nitaendelea tena. Ni sehemu ya kuhifadhi fedha huku ukiendelea kudunduliza ila siyo sehemu ya kutegemea faida kubwa.
 
Biashara nimeshajaribu tatu na zote zilinishinda,ni hela nilipoteza. Kwenye viwanja nakubaliana na wewe,lakini kwenye majengo nadhani ni mada fikirishi bado..Unaweka milion 60 yako kwenye nyumba,je ni lini utaona faida ya hiyo hela ulowekeza?
Sio kila mtu anaweza biashara kama umejaribu biashara tatu na zinabuma. Biashara is not your thing.
 
Mwaka jana biashara ilipamba moto nikaona bora nikomae na biashara niachane na mambo za kuajiriwa

Mwaka huu upepo umegeuka biashara ngumu kuliko jiwe hadi natamani ajira. Nishaurini wakuu

Ninaingiza net profit ya 800k kwa mwezi(hapo nimetoa gharama zote) niendelee kukaza au niajiriwe?
Pesa uliyowekeza NI shilling ngapi?
 
Maisha ya utumishi ni mafupi hivyo ni heri kujiandaa na maisha ya kustaafu mapema.

Kipato vya wafanyakazi wengi ni kidogo sana hivyo kuna ulazima kuwa na kipato cha ziada.

Changamoto ya wafanyakazi wengi ni muda wa kufanya biashara na projects kama kilimo na ufugaji haupo na risk ya kupoteza hela zako ni kubwa kuliko kupata faida sababu ya usimamizi duni.

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa mfanyakazi, hauhitaji muda mwingi,risk ya kupoteza pesa sio kubwa na wenye faida ya kueleweka.

Naongelea vitu kama UTT, treasury bills na Bonds, Hisa kwenye makampuni ya kitaifa na kimataifa na fursa nyingine nyingi na nzuri ambazo mfanyakazi anaweza kujiingiza ili kutunza na kuongeza kipato chake.

Nafahamu humu ndani kuna wataalamu wa mambo ya uchumi na uwekezaji, kuna wawekezaji wakubwa na wadogo, kuna matajiri wa kutosha, njooni mtushike mkono tujue namna gani tunaweza kukuza vipato vyetu vidogo na kuingia kwenye utajiri.
Karibuni.
Good
 
Back
Top Bottom