Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Hii ishu ya ufugaji niliwaza kuifanya kwa large scale,Nitafute eneo kubwa huku mkoani Mara,nijenge mazizi na kijumba cha mchungaji,alafu niweke ng´ombe,mbuzi na kondoo. Ila ishu ya usalama wa hiyo mifugo ndio ilinipa wasiwasi maana inabidi ufuge eneo ambalo halina watu wengi,porini huko kwenye majani mengi.
Pia usimamizi wengi si waaminifu utalizwa
 
Mwajiriwa kama hauna mda wa kusimamia biashara yako achana na kupoteza hela yako.
Wekeza kwenye majengo na viwanja tu, biashara utapigwa hatuna sifa za uaminifu
Biashara nimeshajaribu tatu na zote zilinishinda,ni hela nilipoteza. Kwenye viwanja nakubaliana na wewe,lakini kwenye majengo nadhani ni mada fikirishi bado..Unaweka milion 60 yako kwenye nyumba,je ni lini utaona faida ya hiyo hela ulowekeza?
 
Nyumba kubwa hazilipi,jenga guest,hostel,frame,air b an b,chumba sebule,
 
Maisha ya utumishi ni mafupi hivyo ni heri kujiandaa na maisha ya kustaafu mapema.

Kipato vya wafanyakazi wengi ni kidogo sana hivyo kuna ulazima kuwa na kipato cha ziada.

Changamoto ya wafanyakazi wengi ni muda wa kufanya biashara na projects kama kilimo na ufugaji haupo na risk ya kupoteza hela zako ni kubwa kuliko kupata faida sababu ya usimamizi duni.

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa mfanyakazi, hauhitaji muda mwingi,risk ya kupoteza pesa sio kubwa na wenye faida ya kueleweka.

Naongelea vitu kama UTT, treasury bills na Bonds, Hisa kwenye makampuni ya kitaifa na kimataifa na fursa nyingine nyingi na nzuri ambazo mfanyakazi anaweza kujiingiza ili kutunza na kuongeza kipato chake.

Nafahamu humu ndani kuna wataalamu wa mambo ya uchumi na uwekezaji, kuna wawekezaji wakubwa na wadogo, kuna matajiri wa kutosha, njooni mtushike mkono tujue namna gani tunaweza kukuza vipato vyetu vidogo na kuingia kwenye utajiri.
Karibuni.
Umenikumbusha mbali sana,
Huko nyuma JF tuliwahi kuwa na Chai day, maalumu kwa ajili ya kuongea mambo ya uwekezaji. Siku nzima hakuna kunywa ulabu kwenye mkutano, tuliwahi fanyia mikutano Lunch Time Hotel, Law school of Tanganyika, Luther House, those good days sijui zimepotelea wapi.
 
Muda bro,muda umepita.
 
Nyumba kubwa hazilipi,jenga guest,hostel,frame,air b an b,chumba sebule,
Guest house,hostel na lodge hapa tunaongelea biashara active,hii inahitaji usimamizi wa karibu mkuu. Nyumba za chumba na sebule labda tunahitaji hesabu za mezani,ujenge za Tsh ngapi,unapangisha Tsh ngapi alafu tuone miaka mingapi unapata return ya pesa zako then faida. Kuhusu Air bnb sijaujua huu uwekezaji vizuri.
 
Ni ngumu kuweka 20% ila ni rahisi sana ukiamua. Mi ndo nimejaribu inawezekana . We piga hesabu mshahara wako ni ngapi, kabla ujatoa kulipa madeni kitu cha kwanza ile 20% iwe umesha iweka kando.
Kwa lugha nyepesi kama unalipwa 1000000 unatoa 200000 inayobaki ndo yako tena uandike akilin mwako kwamba mwisho wa mwezi naingiza 800000
 
Guest lodge ni rahisi kusimamia kupitia technology unafunga CCTV camera kujua wangapi wamelala au unafunga sensor kwa bed inakaunti time ya mtu kalala masaa mangapi so kama kitanda hajijaguswa utajua.
Camera ufungwa kwenye corido.
Air b an b ni nyumba mfano wa Uber au bolt unaziweka mtandaoni pana watu au wageni wanakodi chumba kwa siku so inakuwa inaonekana dunia nzima unatoza kwa siku labda sh elf 8 au kumi so inategemea na mgeni anataka kukaa kwa siku ngapi.
Chumba self unajenga mtindo wa cotas, ujenzi wowote unarejesha hela baada ya miaka kumi,jengo ni kutunza pesa na pia ni mtaji siku ukipata mda umestaafu au kazi imeisha unaikopea then unafanya biashara unayoweza kusimamia mwenyewe tofauti na kuwapa watu wasimamie wengine wameandikiwa kuwa umasikini watazika pesa yako utaishia kulipa madeni bure ya mikopo.
 
Umenikumbusha mbali sana,
Huko nyuma JF tuliwahi kuwa na Chai day, maalumu kwa ajili ya kuongea mambo ya uwekezaji. Siku nzima hakuna kunywa ulabu kwenye mkutano, tuliwahi fanyia mikutano Lunch Time Hotel, Law school of Tanganyika, Luther House, those good days sijui zimepotelea wapi.
Watu ni wabinafsi
 
Guest lodge ni rahisi kusimamia kupitia technology unafunga CCTV camera kujua wangapi wamelala au unafunga sensor kwa bed inakaunti time ya mtu kalala masaa mangapi so kama kitanda hajijaguswa utajua.
Camera ufungwa kwenye corido.
Air b an b ni nyumba mfano wa Uber au bolt unaziweka mtandaoni pana watu au wageni wanakodi chumba kwa siku so inakuwa inaonekana dunia nzima unatoza kwa siku labda sh elf 8 au kumi so inategemea na mgeni anataka kukaa kwa siku ngapi.
Chumba self unajenga mtindo wa cotas, ujenzi wowote unarejesha hela baada ya miaka kumi,jengo ni kutunza pesa na pia ni mtaji siku ukipata mda umestaafu au kazi imeisha unaikopea then unafanya biashara unayoweza kusimamia mwenyewe tofauti na kuwapa watu wasimamie wengine wameandikiwa kuwa umasikini watazika pesa yako utaishia kulipa madeni bure ya mikopo.
Uhakika wa soko kwa hizi Air bnb ukoje mkuu?
 
Ni ngumu kuweka 20% ila ni rahisi sana ukiamua. Mi ndo nimejaribu inawezekana . We piga hesabu mshahara wako ni ngapi, kabla ujatoa kulipa madeni kitu cha kwanza ile 20% iwe umesha iweka kando.
Kwa lugha nyepesi kama unalipwa 1000000 unatoa 200000 inayobaki ndo yako tena uandike akilin mwako kwamba mwisho wa mwezi naingiza 800000
Mkuu mimi naweza zaidi ya 20%,kiufupe hela nayotunza ni nyingi kuliko ninayotumia,lakini imewezekana sababu sijawa na majukumu mengi,Nawaza siku ambayo majukumu yatapiga hodi.
 
Back
Top Bottom