JosephNyaga
JF-Expert Member
- Apr 28, 2014
- 291
- 232
Kuna nyimbo hazitakuja kupotea vizazi mpaka vizazi kwa sababu maDJ wanarithishana kadri miaka inavyokwenda mbele. Kuna nyimbo moja ya sebene au rumba ya congo nimeisahau inaitwaje lakini itakuwa imepigwa kqmq sio Wenge Musica/BCBG basi ni Extra Musica. Kuna mahali jamaa anasema "Ayaya msingwemba ayaya ma***** amununyema amununyema amununyemaaaaa" Bonge moja la sebene lililotulea na kutukuza miaka ya 90 huko. Nimetoka kusikia muda huu inapigwa redioni ooohhh walahi nimekumbuka mbali sana utotoni. Anayekumbuka ni wimbo gani atupie hapa tafadhali.