Huu wizi kupitia Tigopesa, naomba Tigopesa mnisaidie majibu hapa

Hakuna namba ya Tanzania inayoanzia na 252, Tanzania namba zinaanzia na 255, nadhani hii iwe ni njia nzuri ya kundua namba feki, ila kitu ninachohisi ni kwamba hiyo meseji haijatoka Tigo pesa, ungekuwa unatumia smartphone ungegunduankwa sababu ingekuja kwenye chat mpya na si ya siku zote toka Tigo pesa, ila kwa kitochi kila namba inaanza na chat mpya, hivyo ni ngumu kujua, ni kwamba ile sehemu ya namba wanaweka jina la Tigopesa, ila hiyo meseji si ya Tigo pesa, either uliwapa simu yako wakasave namba yao kwa jina la TIGOPESA au kuna wafanyakazi wasiowaaminofu Tigo wameisave namba yake kwa jina la TIGO PESA. Na pia ni bora uwe unaangalia salio kila mtu anapotoa pesa
 
Hataki kukiri kama kuna uzembe alifanya, jamaa inaonesha ni wale watu wanaojiona hawawezi kukosea
Hata mi nimegundua ni mtu wa aina hiyo. Waliomshauri aangalie Phone book yake kulitafuta hilo jina ni wengi, lakin kaamua kutojibu.
 
Reactions: amu
Hapo umepigwa siku nyingine MTU akija kutoa pesa nyingi kama umfahamu angalia salio kama limeongezeka,maana usiamini SMS za miamala siku hizi wanatengeneza SMS wakishirikiana na baadhi ya wafanyakazi makao makuu wasio waaminifu kitengo cha pesa mtandao husika
 

Unaweza ukadhani hivyo lkn kwa uzoefu wangu na hii biashara matapeli wanaoibia pesa mawakala na yule wakala mkuu wako.akipita kijana wake wa kutoa huduma ya float mtaani na akakuta ofisi ni mpya au mfanyakazi ni mgeni lazima wampige pesa.

Unaweza kupokea msg imeandikwa gawio,sasa jiulize msg ya gawio inatoka wapi kama sio kwa tigo wenyewe!?ukishapata msg hiyo wanakupigia simu na kuanza kukupa maelekezo mpk unaibiwa.

Wewe jiulize kwann utapeli wote wanaofanyiwa mawakala unafanywa kwenye line ya tigopesa!?ni kwakua huo mtandao una loophole ya mawakala wa wakuu kuibia mawakala wadogo.

Cha msingi hapa muelekeze kijana wako au wewe mwenyewe ukipigiwa siku toka tigo na kuanza kupewa maelekezo sijui commission ndogo sijui tutajie namba yako tukupigie ili tukupe maelekezo ya kufanya kwenye line ya uwakala ujue unapigwa.
 
Hapo umepigwa siku hizi wanatengeneza SMS ya miamala wakishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa mtandao husika ndio maana ushauriwa usiamini SMS siku nyingine angalia salio kwa kama limeongezeka MTU akitoa pesa nyingi kabla kumpa na kumruhusu kuondoka
 
Dawa yao hao ni kuweka cctv camera, watakuibia lakini unauwezo wa kuwapata, tena saiv kuna NIDA. Mfano ni benki ukiwaibia watakupata tu kwa sababu wana ushaidi na video inayowaonesha mwizi wao.
 
mbona namba iliyoleta text zote inaonekana ni TIGOPESA?
Watakuwa walishika simu yake wakasave namba zao kwa jina la TIGOPESA, au kule tigo wanatuma meseji mithili ya zile za tangazo a la ‘AFYA CORONA’ au ‘TATU MZUKA’ ila badala yake wanaandika ‘TIGOPESA’, kama unatumia smartphone utagundua maana utaona inaanza chat mpya na si ya zamani, ila kwa kitochi huwezi jua
 
Washike simu au washike dawa yao ndogo tu angalia salio kabla kuwapa pesa au kuwaruhusu kuondoka usiamini SMS zinaeditiwa siku hizi
 
Hawa watu wanaotapeli hivi wameongezeka sana siku hizi.Wengine ni hawa wa naosema wanaunganisha vifurushi vya chuo kwa bei nafuu
 
Inshu ndogo tuu Mtu akitoa pesa mwambie akuonyeshe message iliyorudi baada ya yeye kutoa pesa unaangalia na muda kabisa
 

Mawakala hawatumii ‘smartphones’ kufanya miamala, nadhani ni maelekezo ya kazi yao.
 
Jamaa anaambiwa aangakie phone book.... Yeye anasema walijuaje salio.... Usijue kuwa Hizi ishu wanacheza n watu w tgo.
Usikute walishasevu Jina TIGOPESA siku nyingi then siku wanakuja kukupiga hela wakawasiliana na watu WA tgo kuuliza huyu chalii Ana salio kiasi gani... Then wakaedit tu
 
Na kumpoteza maboya wakaandika namba 252 badala ya 255.
 
Mawakala hawatumii ‘smartphones’ kufanya miamala, nadhani ni maelekezo ya kazi yao.
Sidhani ka ni maelekezo ya kazi zao... But nadhan kwa kuwa Vito hi vinatunza chaji na pia havina mambo mengi.
Kumbe smartphone Zina mambo mengi... Mtu hawezi nunua smartphone only for transactions
 


hao jamaa wamekufatilia muda mrefu,wakafanikiwa kushika simu yako ya uwakala wakasave hiyo namba kama Tigopesa cha kufanya kwa haraka sana check contact za kwenye hiyo simu yako ya uwakala utakuta hiyo namba imesaviwa kama Tigo pesa ukiona hivyo ujue ushaliwa tayari,

Salio wanapata kwenye hayo mavitabu mnayojaza au anakuja mtu anajifanya katoka Tigo ni mfanyakazi anakuuliza harafu fasta wanajumlisha na mauchafu yao jamaa akikufowadia sms ya muamala wa Tigo pesa inakuja kama Tigopesa kaka pole sana me nishapoteza kama 3.2 ml,

Chakufanya simu yako ya Uwakala piga marufuku hapo ofisini kwako asishike mtu yeyote zaidi ya mhudumu tu, marufuku kutumika kupiga au kupokea sms na ww kazi yako kila mara ni kuclear contact za kwenye hiyo simu hapo umemaliza mchezo

Otherwise Tigo hawatakupa msaada wowote utapoteza muda

Pole sana
 
Mzee tupe mkasa jinsi walivyo chukua 3m
 
Ndio maana nasapoti swala la mtu 1 laini 2 milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…