Huwa inatokea hii

Huwa inatokea hii

madeinmusoma

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
324
Reaction score
387
Umeenda nyumbani kwa mtu, halafu unakutana na toto sumbufu balaa! Hamjawahi kuonana, lakini limeshakuzoea...
Unakuja mwenyewe labda umechomekea shati, nini!! Linaanza kukurukia rukia, mara linakuvuta shati mpaka linachomoka... Mama yake anabaki, "we Junior hebu muache uncle...."

Basi unafika, unakaa sebuleni, linaanza kukusumbua. Mara likupige kibao cha kushitukiza ulikuwa unaangalia zako mbele kwenye TV, mara linakudandia mapajani... Unajibalaguza kuliambia, "haya nenda kwa mama.." Linakutemea mate usoni na mama yake anacheka tu na kukwambia, "Nakwambia leo utakoma!" (Mimi huwa nayafinya kisiri siri). [emoji12][emoji12][emoji12]

Sasa unakuta umeletewa chai na maandazi, toto lipo mbele yako linakuangalia, linataka kuokota andazi. Kwakuwa unaona mikono yake michafu, unaamua kulimegea kipande... Halitaki, linataka zima...! Hujakaa vizuri, limemwaga chakula kwa hasira...! [emoji853][emoji853][emoji853]

Masaa yanaenda, kwenye TV muda wa habari lenyewe linataka kuweka cartoon... Linaanza kulia kwa nguvu, mamaake anasema, "Hebu liwekeeni makatuni yake!" Kipindi hicho wewe unatamani lipigwe balaa...! Hujakaa sawa, unashangaa umepigwa na remote kichwani!! Unageuka kwa hasira, unakuta toto linacheka.... [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ngoja niishie hapa, ila kama upo hivyo na mtoto wako, watu hawapendi..... [emoji36][emoji36][emoji36]
 
Dawa yake ni moja unamkamata unambinya kwa nguvu huku umemkazia macho ya hasira
Nakwambia huyo junior atakuona kama nyoka.
 
Na wewe uende kwa watu kuangalia TV?
 
Mimi huwa napiga makonzi ya kimya kimya than naaga muda huo huo.
 
Hayo matoto ya hivyo mimba zao huwa zinapatikana endapo wazazi watakutana wakiwa tungi
 
Mimi ndio maana sitaki mazoea...nikishaona mtoto mtundu ananisogelea namkata jicho hilo mwenyewe anageuza
 
Back
Top Bottom