Huwa mnakumbuka nini enyi wanaume

Hahah,.expire wangu alinambia hivi "mama nimezunguka naomba unisamehe,naomba unipokee tufunge ndoa" hahhahhaa hakuna siku nilicheka kama ile aisee nikamwambia tuu "samahani Mr sina mpango wa kuolewa leo wala kesho so ww endelea kuzunguka tuu na dunia"....watu za hivi wanashangaza sana duniani jamanii Mimi huwa nawashangaa kwelikweli,.MTU wa hivi namchukulia kama punguani au mgonjwa wa magonjwa yote.
 
Yaani shosti acha tuu,wengine alhamdulillah Allah akitupa wepesi wakusahau tunasahau hadi kucha zao,halafu umesahau mwenyewe umenawiri umenoooga umezidi kuwa mtamm utaliona jitu hilo linakuja kama mtumwa wa zama za pilato anakuangukia,.nyooo unaweza mmwagia tindikali kwa hasira haki vile[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Unazidi kuwa mta.mu......


Hahahahahahhaaaaaa
 
Yaani. Acha tu rafiki
 
Wanaume huwa wanaumia sana wakiona umemove on halafu ukute kule alipojipeleka mlipoachana kunawaka moto basi atataka kujirudisha kwako anapoona kidogo kuna unafuu ila hata akirudi bado ni ngumu yeye kuwa kama zamani kabla hamjaachana atakusumbua sumbua tu.
 
Nilikuwa muumini mkubwa sana wa huo msemo wa 'usirudie matapishi' hadi miaka miwili iliyopita.

Mwaka 2015: Moshi, KLM
Kuna mzee mmoja wakati tunakuwa alikuwa ndo kipimo cha ulevi. Ulevi wake ulikithiri kiasi kwamba alifukuzwa kazi. Alikuwa mwalimu mzuri sana. Wale waliokwenda kusoma huko ulaya enzi za Nyerere. Ulevi wake ulimfanya wakaachana na mkewe.

Mwaka 2015 baada ya kuacha pombe kwa miaka miwili walirudiana na mkewe na tulienda kwenye sherehe yao ya kubariki ndoa. Mpaka ninaandika hapa wapo pamoja na ndugu zangu walio Moshi wanasema wanaishi kwa amani.

Mwaka 2017: huku na kule duniani
Hawa ni wazungu. Walioana kijana akiwa 22 na binti 19. Wakazaa watoto. Baadaye wakashindwana tu. Kijana alikuwa mkorofi tu hakumaliza mambo ya ujana anajisemea mwenyewe. Miaka 30 baadaye, huku kila mmoja akiwa na mtoto wa nje, wamerudiana na wanaishi pamoja.

Mimi: 2008
Nilimpenda binti. Baada ya mimi kumaliza chuo nilienda kufanya kazi mbali na yeye. Alianza kuonesha hints za kushindwa akisema alitamani ule ukaribu kwenye mahusiano. Baada ya muda tukaachana. Miezi michache baadaye nikambembeleza turudiane nikiahidi nitajitahidi kuwa nakwenda kumsalimia. Baada ya kufanya safari mbili, akaniacha akisema ananipenda sana lakini anashindwa. Mara hii, alirudi yeye kutaka tujaribu tena.
Nilipima malalamiko yake ya mwanzo na hali tuliyokuwa nayo nikaona hakuna kilichobadilika. Nilikuwa ninampenda nakuhakikishia. 2009/10 ndo enzi facebook imeshika kasi kweli basi nilikuwa nimemuweka huko kote. Ila nilijua najiset up for maumivu tu, kwa kuwa hakuna kilichobadilika katika kilichotufanya tuwe pamoja. Nilifanya maamuzi ya kutokukubaliana na hilo.

In short, hakuna formula kwenye mapenzi. Cha maana ni kuhakikisha kile kilichofanya muachane kimerekebishwa ama la. It may work kama hao wawili it may not work kama mimi, lakini hakuna matapishi kwenye mapenzi. Ndiyo maana watu wanaoa watu waliokwisha kujifungua hata watoto wawili, wanaoa divorcees.

La pili na la muhimu, unapoamua kurudiana naye, hakikisha mnaanza moja. Mara nyingi wengi hukosea hapa na ku-assume walipoachia. Anza moja kwenye urafiki.

Mwisho, kwako Mama Sabrina, naamini mpaka umeileta hii huku kuna hisia moyoni mwako (unless wewe ni wale wa kuanzisha thread ali mradi uonekane umeanzisha). Do not ignore the feeling, do not fight it...jiridhishe tu uanze moja. Mwisho wa siku tunahitaji kuwa na tumpendaye.
 
awali ni awali hakuna awali mbovu ila kuna wanawake ni watamu mno hadi huwa najiuliza hv tuliachanaje kwa utamu ule alonao sijui nililogwa ndio tukaachana?
 
Kuna ktu alisahau uyoo labdaa. Tafadhar msikilize

Hahahaa uzembe ambao cwez fanyaa
 
kuna rafiki yangu huwa anatibuana na demu wake wanaseparate hadi miezi mi3 na bado wanapendana ila huwa wanategeana nani ataanza kumpigia cmu mwenzake.Cku m1wapo akijitoa ufahamu kuanza kupiga cmu na mapenzi huanza upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…