Huwa mnakumbuka nini enyi wanaume

Huwa mnakumbuka nini enyi wanaume

Hongera
Ila mara nyingi kujinasibu kama huku ni kwa sababu umekuta yaliyomo huko uliko .
Kwa kuwa wapo kama wewe wanaopasha na kula viporo hasa kwa kuwa walipokwenda pana moto ingependeza na kukuona kweli hutiki kurudi kama ungemshirikisha mumeo
 
Nilikuwa muumini mkubwa sana wa huo msemo wa 'usirudie matapishi' hadi miaka miwili iliyopita.

Mwaka 2015: Moshi, KLM
Kuna mzee mmoja wakati tunakuwa alikuwa ndo kipimo cha ulevi. Ulevi wake ulikithiri kiasi kwamba alifukuzwa kazi. Alikuwa mwalimu mzuri sana. Wale waliokwenda kusoma huko ulaya enzi za Nyerere. Ulevi wake ulimfanya wakaachana na mkewe.

Mwaka 2015 baada ya kuacha pombe kwa miaka miwili walirudiana na mkewe na tulienda kwenye sherehe yao ya kubariki ndoa. Mpaka ninaandika hapa wapo pamoja na ndugu zangu walio Moshi wanasema wanaishi kwa amani.

Mwaka 2017: huku na kule duniani
Hawa ni wazungu. Walioana kijana akiwa 22 na binti 19. Wakazaa watoto. Baadaye wakashindwana tu. Kijana alikuwa mkorofi tu hakumaliza mambo ya ujana anajisemea mwenyewe. Miaka 30 baadaye, huku kila mmoja akiwa na mtoto wa nje, wamerudiana na wanaishi pamoja.

Mimi: 2008
Nilimpenda binti. Baada ya mimi kumaliza chuo nilienda kufanya kazi mbali na yeye. Alianza kuonesha hints za kushindwa akisema alitamani ule ukaribu kwenye mahusiano. Baada ya muda tukaachana. Miezi michache baadaye nikambembeleza turudiane nikiahidi nitajitahidi kuwa nakwenda kumsalimia. Baada ya kufanya safari mbili, akaniacha akisema ananipenda sana lakini anashindwa. Mara hii, alirudi yeye kutaka tujaribu tena.
Nilipima malalamiko yake ya mwanzo na hali tuliyokuwa nayo nikaona hakuna kilichobadilika. Nilikuwa ninampenda nakuhakikishia. 2009/10 ndo enzi facebook imeshika kasi kweli basi nilikuwa nimemuweka huko kote. Ila nilijua najiset up for maumivu tu, kwa kuwa hakuna kilichobadilika katika kilichotufanya tuwe pamoja. Nilifanya maamuzi ya kutokukubaliana na hilo.

In short, hakuna formula kwenye mapenzi. Cha maana ni kuhakikisha kile kilichofanya muachane kimerekebishwa ama la. It may work kama hao wawili it may not work kama mimi, lakini hakuna matapishi kwenye mapenzi. Ndiyo maana watu wanaoa watu waliokwisha kujifungua hata watoto wawili, wanaoa divorcees.

La pili na la muhimu, unapoamua kurudiana naye, hakikisha mnaanza moja. Mara nyingi wengi hukosea hapa na ku-assume walipoachia. Anza moja kwenye urafiki.

Mwisho, kwako Mama Sabrina, naamini mpaka umeileta hii huku kuna hisia moyoni mwako (unless wewe ni wale wa kuanzisha thread ali mradi uonekane umeanzisha). Do not ignore the feeling, do not fight it...jiridhishe tu uanze moja. Mwisho wa siku tunahitaji kuwa na tumpendaye.
Miaka 30 baadae ni mingi kweli.
 
Mwanaume alikuacha akasema atakupotezea muda tu ukipata mtu wa kuwa nae au kuolewa nae olewa tu,,hapo ashakuudhi ashakuumiza ,kweli unavumilia unapata mwingine sasa ,,mnakaa inapita miaka 5 au 6 unashangaa huyo mwanaume anaanza kukutafuta na kupiga piga simu kila muda,na sms haziishi hivi huwa mnasahau nini na mnakumbuka nini nyinyi viumbe muitwao wanaume,yaan mtu nishakusahau hata dudu yako siikumbuki kabisa unaanza kujirudisha rudisha na kusema nina mpango naupanga sijui nin nanii ooh mara huwa nakukumbuka sana,nakufikiria Mama sabrina yaishe hayo,Mimi sirudi nyuma naenda mbele huko huko sirudii matapishi kabisa,maana kurudia rudia vitu ya zamani ni kujichosha tu tena mtu alikupa maudhi bora hata kama mliachana kwa wema tu.
Hapa namkaushia tu nataka nimuulize hivi ulisahau nin kwa mama Sabrina au anaumwa huyu mtu ,itakuwa anaharisha kabisa,kaenda kupata kasichana kapuuzi puuzi huko kabayaa wameshindwana huko ujirudishe kwangu marufuku
Mlipoenda muwe mnatulia huko huko msijifanye kurudi ladha ike ya mwanzo ishaisha kabisa ,tunataka wapya tu wa kuanza nao upya

Mario kakosa kwa kuhemea, anataka kurudi nyumbani kusubiri chakula cha kuitiwa kwa kupigiwa kengele.
 
kuna rafiki yangu huwa anatibuana na demu wake wanaseparate hadi miezi mi3 na bado wanapendana ila huwa wanategeana nani ataanza kumpigia cmu mwenzake.Cku m1wapo akijitoa ufahamu kuanza kupiga cmu na mapenzi huanza upya

WARNING: Kuna hangover ya mapenzi.

Waambie wasome kitabu cha TOO GOOD TO LEAVE, TOO BAD TO STAY.

Yaani kuna vitu vizuri kwa huyo mtu inakuwia ngumu kuachana naye na bado kuna vitu vibaya (ambavyo hukubaliani navyo principally) ambavyo ni afadhali muachane.

Hawa wasipofanya maamuzi magumu watakuja kuumia sana mbeleni (actually mmoja wapo atakuja kuumia sana mbeleni).

AU

Utoto! Ni watoto bado wakikua watasuluhisha tofauti zao wasonge mbele pamoja. Ingawa hii siipi nafasi sana.

Anyway, ningejua vyema ningeweza kusema zaidi. Waweza kuwa na mfano wa jambo ambalo huwatenganisha?

Nina wasiwasi sana mmojawao atakuja kuumia. Kuna mmoja ameshajua mwenzake anampenda. Wakiachana, siku akiwa mpweke atamtafuta. Siku huyu mwingine akiwa mpweke naye akitafutwa anakubali maana amin amin nakuambia, hakuna asiyependa free p!
 
Miaka 30 baadae ni mingi kweli.

Ni kweli kabisa. Sikuamini ila kwa kuwa waliokuwa wananieleza ni wao wenyewe nilikubali. Walinieleza hayo huku wakinionesha picha zao. Na wote wakaenda huko nje wakazaa watoto halafu kichekesho sasa watoto hao wote wana jina linalofanana.

Ni kweli mara nyingi (tena hii niisisitizie: MARA NYINGI) mahusiano ya kurudiana huwa hayafiki mbali hasa kwa kuwa kilichofanya watu waachane hakijashghulikiwa. Lakini mkiwa matured enough na mkaona mmesharekebisha kilichowatenganisha kwa nini msirudiane. Aisee, nilikuwa napenda kweli kujisemea sirudii matapishi lakini baada ya hayo nimegundua mapenzi ni kitu kingine..CHA MAANA NI KUWA MAKINI THE SECOND TIME!!!!
 
Second chance mara nyingi haziaminiki. Mimi mwenyewe nimeshakua mhanga wa hilo jambo ila juzi nimeona hapana niendelee na maisha mengine mapenzi nitakutana nayo kwingine.
 
Mwanaume alikuacha akasema atakupotezea muda tu ukipata mtu wa kuwa nae au kuolewa nae olewa tu,,hapo ashakuudhi ashakuumiza ,kweli unavumilia unapata mwingine sasa ,,mnakaa inapita miaka 5 au 6 unashangaa huyo mwanaume anaanza kukutafuta na kupiga piga simu kila muda,na sms haziishi hivi huwa mnasahau nini na mnakumbuka nini nyinyi viumbe muitwao wanaume,yaan mtu nishakusahau hata dudu yako siikumbuki kabisa unaanza kujirudisha rudisha na kusema nina mpango naupanga sijui nin nanii ooh mara huwa nakukumbuka sana,nakufikiria Mama sabrina yaishe hayo,Mimi sirudi nyuma naenda mbele huko huko sirudii matapishi kabisa,maana kurudia rudia vitu ya zamani ni kujichosha tu tena mtu alikupa maudhi bora hata kama mliachana kwa wema tu.
Hapa namkaushia tu nataka nimuulize hivi ulisahau nin kwa mama Sabrina au anaumwa huyu mtu ,itakuwa anaharisha kabisa,kaenda kupata kasichana kapuuzi puuzi huko kabayaa wameshindwana huko ujirudishe kwangu marufuku
Mlipoenda muwe mnatulia huko huko msijifanye kurudi ladha ike ya mwanzo ishaisha kabisa ,tunataka wapya tu wa kuanza nao upya

1. Nakumbuka uliitisha interview about a week or two weeks ago
2. Then Nakumbuka uliitwa Catalunya ukamtosa jamaa cz alizidiwa na wenzie

Nisaidie results za Na. 1 and Na. 2 then ntakushauri what to do with the dude
 
Unaniandalia season sio[emoji6][emoji6][emoji6][emoji6]
 
Back
Top Bottom