Hayo wenye anga zao wanayaita mataputapu! Pombe gharama mzee! Chupa moja ya beer baa za kawaida 2,000 mpaka upate sitimu unahitaji angalau vyupa 5 hapo 10,000 ambayo kwa mwezi ni 300,000/. Tena huyu ni mnywaji wa kujibana. Kuna whisky chupa moja bei 150,000 hadi 300,000/. Kwa wanaopenda totoos michepuko savanna moja 4,000/ baa za kawaida na totoos atakunywa kama 8 hivi bill 32,000 bado chakula na mambo mengine! Hata hivyo akili ya kupata michongo ya hela inapatikana kutokana na aina ya watu unaojumuhika nao. Huyu atakunywa vinywaji (vilevi) vya bei lakini ana nafasi kubwa ya kupata michongo ya kumuingizia hela zaidi kiasi kwamba pesa anayotumia kunywa ni ndogo sana (negligible). Wewe unayekunywa mataputapu hebu geuka kulia na kushoto angalia aina ya watu unaojumuika nao! Je! Hao njemba watakupa wazo gani la kukusaidia? Acha mataputapu kijana! Jiongeze jumuika na wasure! Kalaghabaho!