Huwa mnazitatuaje changamoto kama hizi?

Huwa mnazitatuaje changamoto kama hizi?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Yaani kuna wakati unakuwa na watu wa karibu zaidi ya mmoja lakini unakuta kuna mmoja anamzunguka mwenzake na kufanya vitu viovu au kumsaliti huku wewe ukiwa unajua kabisa.

Kwa mfano, huku mtaani unakuwa na rafiki yako lakini ukawa unajua kabisa kwamba mke au mme wake anamsaliti au amezaa nje ya ndoa huku mmoja wapo akiwa hajui

Je, uliwahi kuingia kwenye changamoto kama hizo na uliamua kuongea au ulikaa kimya tu mpaka maji yalipo mwagika yenyewe.
 
Kaa kimya mkuu achana na watu wanaojifunika shuka moja utamwambia kwa uzuri tu mwisho wa siku ubaya wote unakuangukia wewe utaanza kuulizwa mambo ya ushahidi una uhakika unabaki kujiuma uma

Kama kazaa nje au wanasalitiana za mwizi arobaini watakamatana wenyewe tu
 
Back
Top Bottom