Huwa nawaza mengi kuhusu utengenezwaji wa fedha

Hata kama serikali ingeprint pesa nyingi unadhani ndio kigezo cha kila mtu kupata pesa? Kwa akili yako unadhani serikali inagawa pesa? Fanya kazi upate pesa.

Huo mgao wa fedha unaouwaza athari zake ni pamoja na kudumaza shughuli za kiuchumi uzalishaji utapungua,watu hawatatafuta pesa tena kwakuwa yukonazo amezifungia tu stoo.
 
UNIQUEMAN1,

Hicho unachosema ni dhambi kubwa kwenye uchumi. Nchi ikifikia ku print fedha na kuingiza kwenye mzunguuko wake literally it commits economical suicide.

Pesa ya nchi inatengenezwa kwa mahesabu makali sana na udhibiti wa hali ya juu kwa uwiano wa rasilimali zake. Baadae watakuja wataalam wa uchumi humu kukufafanulia na kudadavua zaidi

Uganda iliwahi kufanya hivyo enzi za Rais Idd Amin Dada na matokeo yake fedha yake ikawa haina thamani kabisa.

Hata "mabeberu" wakitaka kuwahujumu kiuchumi wana print pesa zenu kwa wingi kisha wanazipenyeza kwenye mzunguuko wenu wa uchumi/fedha kama walivowafanyia Zimbabwe wakati wa Mugabe. Matokeo yake ikawa bei ya mkate mmoja ni paund za Zimbabwe milion kumi!!!
 
Fikiria pesa zichapwe na kila mtanzania apewe bilioni 5 - jee kuna bidhaa za kutosha kununuliwa nchini na mabilionea wa shilingi wote hawa?

Jee kuna atakayehangaika na jembe la mkono kuzalisha mahindi, kuvua, nk?

Ya Zimbabwe yatatokea ambapo ndizi 1 itauzwa sh laki 5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutakuwa kama zimbabwe. Lazima kuwe na kitu kama BOT ndio regulator authority. Hapo wakigusanisha nyaya vibaya. Tutakwenda kununua azam cola na gunia la hela.
😂😂😂😂😂😂😂
 
Kupitia benki kuu ambaye ndiye kiongozi wa benki zote pesa zote chakavu zinazo kusanywa na benki zote nchini uludishwa benki kuu na kuhesabiwa Kisha uchomwa Moto na kiasi kile kile Cha pesa utengenezwa upya nakuludishwa kwenye mzunguko.

Hakuna kuongeza ata Senti tano hapo. Pia serikali ikiona Kama pesa imekuwa nyingi kwenye mzunguko uwamua kuwakopa wananchi wake kwa kutoa Bondi za serikali ambapo wananchi uzinunua na muda wa kulipwa ukifika serikali uwalipa pesa yao pamoja na riba.

Pesa ikiwa chache kwenye mzunguko serikali uanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo Kama vile ujenzi wa barabara, reli, madaraja, vituo mbalimbali vya afya na tenda upewa kampuni binafsi ili ziajiri vibarua na wafanyakazi kutoka mitaani ili wajipatie kipato hvyo kuongeza pesa kwenye mzunguko.
 
Nimekumbuka kitu kinaitwa demand and supply, more money and goods scarcity.
 
Pesa iendane na kiwango cha uzalishaji mali.
 
Fedha ina thamani ya uhalisia zaidi ya ile ambayo imepewa na binadamu thamani ambayo ya kufikirika tu ?

Mimi nina ngano nataka mchele naenda kwa mtu mwenye mchele nampa ngano kilo moja ananipa mchele nusu,huu ni muamala ambao ungefanyika kwa pesa.

Katika muamala kama huu thamani ya pesa inaonekana wapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M Kuu safuher hilo liliwezekana zamani wakati dunia ilikua na wakazi wachache. Kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia sasa hivi inakua changamoto kuendelea kutumia barter trade.

Nakwenda super market kununua bidhaa tofauti tofauti sio rahisi nimebebe vitu mbadala vya kubadilisha. Na pia huyo muuzaji anahitaji vitu nilivyokua navyo mimi? Mizani ya thamani ya vitu tunavyobadilishana itaamuliwaje?

Kuna sekta ya huduma. Nakwenda hotelini nahitaji chumba cha kulala au naenda kwenye usafiri iwe wa nchi kavu, majini au angani napo pia ingehitajika kubadilishana bidhaa kwa bidhaa?

Matumizi ya pesa (media of exchange) ni muhimu na yamekuja kurahisisha miamala kati ya watu, nchi na dunia kwa ujumla. Labda baadae ije mbadala rahisi zaidi kutumia zaidi ya pesa kama ambavyo tunasikia kuhusu non cash transactions(elecrotic transactions) zinavyotiliwa mkazo siku hizi
 
Mkuu hayo yote yanatokea kwa sababu pesa imetiliwa nguvu na umuhimu mkubwa na watu.

Lakini kiukweli pesa bila kupewa umuhimu huo ni jambo linawezekana kutokuwepo kwa pesa.

Kwa mfano super market akiweka utararibu wake kuwa ice cream unanunua kwa mswaki.
Ngano kwa mchele
Soda kwa tende ,Hayo yanawezekana yote kwa sababu hata super market penyewe ukienda unakuta kila kitu na bei yake kwa hyo wewe unaangalia tu kitu hiki bei gani na unaangalia kama unayo na kama hukujipanga utakuja siku nyingine.

Hali kadhalika kwa burter trade inawezekana mtu akaweka bidhaa na kitu cha kubadilishana nacho na mtu akajipanga na hivyo vitu vyake akaenda na huduma ikatokea vizuri tu.

Ila sasa haijapewa umuhimu ndo mana unaona ni ngumu sana,laiti ingepewa umuhimu basi ingeliwezekana.

Mtu unataka kusafiri kwenda oman unakuta tangazo pale kwenda omani nauli ni mchele kilo 20 na kurudi ni mchele kilo 20.kwa hyo yiketi ya kwenda na kurudi mchele kilo 40 zinaenda kuwekwa store,then mchele unaendelea kuzunguka kwingine na kuliwa.

Haya ni mambo yanawezekana.

Pesa sio kitu muhimu katika maisha ila kimepewa umuhimu na kuvaa uhusika feki tu ambao umevishwa na watu.

Leo tuseme pesa zote ziyayuke maisha yataenda vizuri tu,ila jaribu useme mazao na mashamba yayeyuke na viwanda vyote alafu tubaki watu na pesa tu maisha yataendaje ?

Maisha hayawezi kwenda kwa sababu pesa haina umuhimu wowote ule bali imepewa umuhimu tu.

Nduo maana pesa haikutengeneza mashine bali mashine ndo imetengeneza pesa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yoyote ina uwezo wa kuprint pesa zake, seriikali zote duniani zimekua zikifanya hivyo, tatizo ukiprint hela huku hakuna uzalishaji hiyo hela inakua haina thamani tena.

Njia rahisi ya kuelewa kitu kama hiki, ukiwa jangwani hakuna maji, kikombe kimoja cha maji utaona kitu cha muhimu sana, utafanya chochote kile upate hayo maji, ila ukikaa sehemu maji fresh yamejaa unaharibu hata huoni tatizo lolote, mtu akikwambia umfanyie kitu flani akupe maji utamuona chizi, hela iiko hivyohivyo ukiprint nyingi ukagawa kwa kila mtu inakua haina thamani tena, hakuna nchi itataka kupokea hela yako, na vitu itabidi vipande sana bei maana demand imezidi supply, kila mtu anauwezo wa kununua chochote, angalia Zimbabwe walichokifanya wakaishia kununua mkate moja mabilioni, au Venezuela.

Wakati huu wa corona nchi nyingi zinaprint sana hela, kama marekani juzi tu imetoka kuprint $6Trillion ili igawe kwa small businesses wasifukuze wafanyakazi, Tanzania tukiprint kiasi hicho kufikia wiki ijayo tutaamka mkate moja unauzwa laki mbili, marekani hela yao inashuka thamani ndiyo ila inatumia dunia nzima ndiyo maana haishuki thamani sana ukilinganisha na nyingine.
 
Vipi miradi ya maendeleo tenda wakipewa wachina..Kuna impact kiuchumi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu vipi kuhusu hii kitu wanaita quantitative easing hivi na huku kwetu huwa inatumika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…