Mkuu hayo yote yanatokea kwa sababu pesa imetiliwa nguvu na umuhimu mkubwa na watu.
Lakini kiukweli pesa bila kupewa umuhimu huo ni jambo linawezekana kutokuwepo kwa pesa.
Kwa mfano super market akiweka utararibu wake kuwa ice cream unanunua kwa mswaki.
Ngano kwa mchele
Soda kwa tende ,Hayo yanawezekana yote kwa sababu hata super market penyewe ukienda unakuta kila kitu na bei yake kwa hyo wewe unaangalia tu kitu hiki bei gani na unaangalia kama unayo na kama hukujipanga utakuja siku nyingine.
Hali kadhalika kwa burter trade inawezekana mtu akaweka bidhaa na kitu cha kubadilishana nacho na mtu akajipanga na hivyo vitu vyake akaenda na huduma ikatokea vizuri tu.
Ila sasa haijapewa umuhimu ndo mana unaona ni ngumu sana,laiti ingepewa umuhimu basi ingeliwezekana.
Mtu unataka kusafiri kwenda oman unakuta tangazo pale kwenda omani nauli ni mchele kilo 20 na kurudi ni mchele kilo 20.kwa hyo yiketi ya kwenda na kurudi mchele kilo 40 zinaenda kuwekwa store,then mchele unaendelea kuzunguka kwingine na kuliwa.
Haya ni mambo yanawezekana.
Pesa sio kitu muhimu katika maisha ila kimepewa umuhimu na kuvaa uhusika feki tu ambao umevishwa na watu.
Leo tuseme pesa zote ziyayuke maisha yataenda vizuri tu,ila jaribu useme mazao na mashamba yayeyuke na viwanda vyote alafu tubaki watu na pesa tu maisha yataendaje ?
Maisha hayawezi kwenda kwa sababu pesa haina umuhimu wowote ule bali imepewa umuhimu tu.
Nduo maana pesa haikutengeneza mashine bali mashine ndo imetengeneza pesa.
M
Kuu safuher hilo liliwezekana zamani wakati dunia ilikua na wakazi wachache. Kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia sasa hivi inakua changamoto kuendelea kutumia barter trade.
Nakwenda super market kununua bidhaa tofauti tofauti sio rahisi nimebebe vitu mbadala vya kubadilisha. Na pia huyo muuzaji anahitaji vitu nilivyokua navyo mimi? Mizani ya thamani ya vitu tunavyobadilishana itaamuliwaje?
Kuna sekta ya huduma. Nakwenda hotelini nahitaji chumba cha kulala au naenda kwenye usafiri iwe wa nchi kavu, majini au angani napo pia ingehitajika kubadilishana bidhaa kwa bidhaa?
Matumizi ya pesa (media of exchange) ni muhimu na yamekuja kurahisisha miamala kati ya watu, nchi na dunia kwa ujumla. Labda baadae ije mbadala rahisi zaidi kutumia zaidi ya pesa kama ambavyo tunasikia kuhusu non cash transactions(elecrotic transactions) zinavyotiliwa mkazo siku hizi
Sent using
Jamii Forums mobile app