Huwa unasoma na kuelewa Sera ya Faragha (Privacy Policy) kabla ya kukubali (Accept)?

Huwa unasoma na kuelewa Sera ya Faragha (Privacy Policy) kabla ya kukubali (Accept)?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Sera ya faragha (Privacy Policy) ni maelezo ya kina kuhusu jinsi taarifa binafsi zinavyokusanywa, zinavyochakatwa, kutumika na kulindwa katika programu ya simu au tovuti husika.

1728555595725.png
Wengi wetu hukubali sera za faragha bila kuzisoma, lakini n muhimu kupitia sera za faragha za tovuti na programu unazotumia ili kuelewa jinsi taarifa zako zinavyokusanywa na kuchambuliwa

1728555676971.png
Wakati mwingine sera za faragha hutumika na Wadukuzi ili kuweza kupata taarifa zako binafsi na kufanya ulaghai mtandaoni, uwizi wa utambulisho na vitendo vingine vya kihalifu mtandaoni
 
Ujue saa zingine tusidanganyane wala kuonana wazembe au wavivu. Hizo terms of service na privacy policy ni vitu vya kitaalamu sana na mara nyingi ili uelewe unahitajika kuwa na mtu aliyebobea kwenye maswala hayo akuchambulie/akutafsirie kimoja kimoja. Kuna lugha za kisheria, kimtandao, na mambo mengine ya kiTEHAMA TEHAMA. Kibongo chenyewe tu mtihani ndio itakuwaje kiprince hicho!

Tatizo na wao wameshalijua lipo wapi na ndiyo maana hutakuta wamekuwekea kwa lugha yako.
 
Back
Top Bottom