Wakuu kila nyumba ina harufu ambayo wakazi wameizoea na kuhisi kawaida, ila mgeni ukiingia ndio utaiskia kama ni nzuri au mbaya, iwe ya marashi au uvundo. Kuna nyumba zinanukia vizuri sana, harufu murua sana hutatamani kutoka ukiingia.
Kuna njia za Kiasili ambazo wengine hutumia kwenye nyumba zao hata kama hawana uwezo wa kununua marashi ya dukani ya gharama kwa ajili ya nyumba zao.
Baadhi ni kama hizi
Maganda ya machungwa au limao
Chemsha maji kwenye sufuria ndogo kisha weka maganda ya machungwa au limao, vijiti vya mdalasini (cinnamon), na iliki. Harufu yake itatanda nyumba nzima haraka sana.
Kama unapenda harufu ya kahawa
Weka chembechembe za kahawa ya kusaga kwenye bakuli ndogo na uziweke sebuleni au jikoni. Inanyonya harufu mbaya na kuacha harufu nzuri ya asili.
Baking Soda
Hii ni nzuri kwa kunyonya harufu mbaya. Unaweza kuimwagia kidogo kwenye kochi au zulia kabla ya kufanya usafi (fagia au vuta na vacuum cleaner baada ya dakika 15).
Wewe nyumbani kwako unatumia kitu gani kuifanya inukie vizuri wakati wote?