Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 11,050
- 31,412
Kupitia andiko hili kwenye Biblia, mfano alioutoa Yesu dhidi ya tajiri mkulima aliye fikia kilele cha mafanikio ilimchukiza Mungu na kuamua kumuua.
Nimetafakari namna tunavyo ishi sisi wanadamu na utafutaji wetu usiofikia kikomo, leo mtu anaweza kuwa na hatua fulani kwenye maisha yake ambayo ameipigania muda mrefu lakini kesho akatamani hatua nyingine asiyo kuwa nayo.
Tunaweza kusema hatipaswa kuridhika, na pale tu tutakapo ridhika yataweza kutukuta kama ya huyo ndugu aliye tolewa mfano na Bwana Yesu.
Au tusema Mwenyezi Mungu ametuweka hapa duniani kwa madhumuni ya kuendelea kutaabika wakati wote, nikiendelea kutazama huo mfano wa huyo tajiri.
Tuendelee kuweka nia na jitihada katika utafutaji bila kufikia kilele cha kufanikiwa itakayo zaa furaha.
Lakini najiuliza kulikua na sababu gani haswa za Mungu kumuua huyo tajiri mkulima.