Huwenda ikawa mwanadamu hapaswi kuwa na furaha ya maisha moja kwa moja

Huwenda ikawa mwanadamu hapaswi kuwa na furaha ya maisha moja kwa moja

Kiufundi zaidi,.
Hii dunia haina maana yeyote kwa binadamu hata kwa Mungu aliyeifanya kuwepo.

Mungu mwenyewe anaichukia sana na hata binadamu wake wanamchukia sana Mungu mwenyewe.

Binadamu amekuwa mtu wa kumkosea Mungu wake kila kukicha na Mungu pia amekuwa wa kutoa hukumu kila uchwao, huku akisisitiza adhabu ya kiwango cha juu kwa binadamu wake na matendo yao.

Hii ina maana gani!.
Hii ina maana kuwa mambo ya dunia hayako sawa kabisa.
Kweli kabisa ndugu yangu ni kitu wengi wetu hatuwezi kusema hadharani au hata ndani ya dhamiri zetu ila kweli mwadamu hampendi mungu , inaweza pia kuwa hivyo kwa mungu kwa sababu mungu alimshusha shetani duniani na kutahadharisha mwanadamu kwamba usalama wake utakuwa mdogo kwa vile shetani amekuja duniani.
Uwezekano wa mwanadamu kukabiliana na shetani haupo, lakini alishushwa hivyo hivyo na nguvu zake lakini sheria na adhabu anapewa mwanadamu.
 
Kupitia andiko hili kwenye Biblia, mfano alioutoa Yesu dhidi ya tajiri mkulima aliye fikia kilele cha mafanikio ilimchukiza Mungu na kuamua kumuua.

View attachment 3146861

Nimetafakari namna tunavyo ishi sisi wanadamu na utafutaji wetu usiofikia kikomo, leo mtu anaweza kuwa na hatua fulani kwenye maisha yake ambayo ameipigania muda mrefu lakini kesho akatamani hatua nyingine asiyo kuwa nayo.

Tunaweza kusema hatipaswa kuridhika, na pale tu tutakapo ridhika yataweza kutukuta kama ya huyo ndugu aliye tolewa mfano na Bwana Yesu.

Au tusema Mwenyezi Mungu ametuweka hapa duniani kwa madhumuni ya kuendelea kutaabika wakati wote, nikiendelea kutazama huo mfano wa huyo tajiri.

Tuendelee kuweka nia na jitihada katika utafutaji bila kufikia kilele cha kufanikiwa itakayo zaa furaha.

Lakini najiuliza kulikua na sababu gani haswa za Mungu kumuua huyo tajiri mkulima.
[emoji1]
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
Uwezekano wa kudhibitisha pasipo mashaka sina ila wengi wape.
6ac5205bf6da6c8e6467e8e98fb5283b.jpg

Wewe umeweza kujitenga nao ingawa ni wengi pale ulipoona hawako sahihi.
Lakini pamoja kupotoka kwao kwa wingi wao dharura yoyote ikiwapata ni vyepesi wao kuikabili kuliko wewe ulieona usahihi ukiwa peke yako.
 
Kwa nini iwe hivyo sasa, maana ya maisha na uhai ninini kama haipaswi kuwa na amani sambamba na uhai.
Km unaamini katika uwepo wa Mungu na uumbaji utajua binaadam tumeletwa duniani kuwa tested.
Na kujaaliwa akili ya kuchanganua mambo ndio mateso hapo yanapoanzia.
Na kila ukitaka kujua mambo meeengi ndio mateso yanavyozidi. Wakati mwengine bora ujifanye mbumbumbu walau utaishi kwa amani
 
Uwezekano wa kudhibitisha pasipo mashaka sina ila wengi wape.
View attachment 3147630
Wewe umeweza kujitenga nao ingawa ni wengi pale ulipoona hawako sahihi.
Lakini pamoja kupotoka kwao kwa wingi wao dharura yoyote ikiwapata ni vyepesi wao kuikabili kuliko wewe ulieona usahihi ukiwa peke yako.
Wengi wape is a logical fallacy, argument from popularity.

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Km unaamini katika uwepo wa Mungu na uumbaji utajua binaadam tumeletwa duniani kuwa tested.
Na kujaaliwa akili ya kuchanganua mambo ndio mateso hapo yanapoanzia.
Na kila ukitaka kujua mambo meeengi ndio mateso yanavyozidi. Wakati mwengine bora ujifanye mbumbumbu walau utaishi kwa amani
Katika hali ya kawaida ubongo au akili ya binadamu ipo kwa mfumo wa kudadisi na kujifunza, haiwezekani kamwe kujifanya mjinga usiye juwa kitu wala kujishughulisha kujua vitu vipya katika mazingira yanayo mzunguka mtu.

Mimi ni muamini katika dini.
Definition maisha ya mtu au sababu ya uwepo wa mtu katika dunia dini yetu inasema Mungu alituumba ili tumjue, tumtumikie na kurudi kwake, na si alituumba ili tuwe kwenye mitihani tuweze kushinda au kushindwa.
 
Back
Top Bottom