Huwenda ikawa mwanadamu hapaswi kuwa na furaha ya maisha moja kwa moja

Kweli kabisa ndugu yangu ni kitu wengi wetu hatuwezi kusema hadharani au hata ndani ya dhamiri zetu ila kweli mwadamu hampendi mungu , inaweza pia kuwa hivyo kwa mungu kwa sababu mungu alimshusha shetani duniani na kutahadharisha mwanadamu kwamba usalama wake utakuwa mdogo kwa vile shetani amekuja duniani.
Uwezekano wa mwanadamu kukabiliana na shetani haupo, lakini alishushwa hivyo hivyo na nguvu zake lakini sheria na adhabu anapewa mwanadamu.
 
[emoji1]
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
Uwezekano wa kudhibitisha pasipo mashaka sina ila wengi wape.

Wewe umeweza kujitenga nao ingawa ni wengi pale ulipoona hawako sahihi.
Lakini pamoja kupotoka kwao kwa wingi wao dharura yoyote ikiwapata ni vyepesi wao kuikabili kuliko wewe ulieona usahihi ukiwa peke yako.
 
Kwa nini iwe hivyo sasa, maana ya maisha na uhai ninini kama haipaswi kuwa na amani sambamba na uhai.
Km unaamini katika uwepo wa Mungu na uumbaji utajua binaadam tumeletwa duniani kuwa tested.
Na kujaaliwa akili ya kuchanganua mambo ndio mateso hapo yanapoanzia.
Na kila ukitaka kujua mambo meeengi ndio mateso yanavyozidi. Wakati mwengine bora ujifanye mbumbumbu walau utaishi kwa amani
 
Wengi wape is a logical fallacy, argument from popularity.

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Katika hali ya kawaida ubongo au akili ya binadamu ipo kwa mfumo wa kudadisi na kujifunza, haiwezekani kamwe kujifanya mjinga usiye juwa kitu wala kujishughulisha kujua vitu vipya katika mazingira yanayo mzunguka mtu.

Mimi ni muamini katika dini.
Definition maisha ya mtu au sababu ya uwepo wa mtu katika dunia dini yetu inasema Mungu alituumba ili tumjue, tumtumikie na kurudi kwake, na si alituumba ili tuwe kwenye mitihani tuweze kushinda au kushindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…