Huwezi kumaliza tatizo kama hutaki kuwa mkweli, Mwigulu unatuonaje?

Huwezi kumaliza tatizo kama hutaki kuwa mkweli, Mwigulu unatuonaje?

vnn

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
3,030
Reaction score
7,500
Unaposema nchi zinatuonea wivu ndio maana zinachochea fujo unakua unatuona hatuna akili au?

Malalamiko ya watanzania yanajulikana

Hawataki utekaji, hawataki ufisadi na kufuja hovyo mali za umma, hawataki chaguzi za kiini macho wanataka tume huru, wanataka katiba mpya!

Wameongea haya mambo mara ngapi na mkaziba masikio? Watu wana tuhuma nzito za ufisadi ila hawajai kuitwa hata kuhojiwa, watu wana tuhuma za utekaji ila wanatamba tu,

Je hayo mataifa ya nje ndio yanateka watu?

Mataifa ya nje ndio yamekataa kuleta katiba mpya?

Mataifa ya nje ndio yamegoma kuleta chaguzi huru?

Huo ufisadi nchini Tanzania unafanywa na wamataifa ya nje?

Mbona mnamuona kila mtu ni mjinga?

Mnashindwa kukili ukweli na kuyafanya yale wananchi wanayataka mnasingizia watu wa nje?

Dunia ya sasa huwezi kuemdesha nchi kwa propaganda amini hivyo
 
Mwigulu ni waziri mkuu mjinga kuwahi kutokea hapa TZ.Siku si nyingi serikali batili inaondoka madarakani.
 
Yaani huyu jamaa, katangulizwa,nae anaenda kichwa kichwa..bro tuliza fuvu hilo..ISSUE hii ni NZITO!
 
Ni kama wanajibagaza wenyewe kwa kukichanganya kwenye press zao
 
Bora asinge ongea!
Kipi hatujakiona kwenye mauaj na ubakaj?

Maisha na mali kipi kinatangulia?
Angekausha zake tu, ni ngum sana kuisafisha hii serikali kwa sasa!
 
Mwigulu anatuona sisi mafala kama walivyo wanaccm wote. Hatuhitaji mtu kutoka nje aje atuambie kuwa wakosoaji wa Serikali wanatekwa na kuuwawa na dola, hatuhitaji mtu kutoka nje kutuambia kuwa demokrasia hapa Tanzania inabakwa kwa kuendesha chaguzi za maigizo, hatuhitaji mtu kutoka nje ya nchi kutuambia kuwa Taifa letu linatafunwa na gonjwa sugu la rushwa na ufisadi unaofanywa na watawala. Na nchi inayonyooshwa kidole ni 🇰🇪 hivi kweli Kenya wanatuonea wivu kwa kitu gani hasa ilhali uchumi wao ni bora zaidi ya wa kwetu? Bajeti ya Kenya ni mara mbili na nusu ya bajeti yetu sisi hawa ndiyo watuonee wivu sisi ? Mwigulu Nchemba punguza uchawa vinginevyo tutaona PhD yako ni sawa na Msukuma au Babu Tale, jiheshimu na ukome kutufokea.
 
Back
Top Bottom