Huwezi kupambana na Kassim Dewji ukabaki salama

makolo mkijaribu kumtoa babra na mp anasepa,ujanj a wa kumtoa chaunabe hamna
 
Na kingine wasichokijua wengi hapa ni kwamba Kassim Dewji ndiyo Mwalimu wa ule Umafia wote waliokuwa wakiona Marehemu Hanspoppe akiufanya na hajaishia hapo tu bali ni huyu huyu Kassim Dewji ( KD ) au Mvaa Mabomu ya Kipalestina kama Watu wake wa Karibu ( Washkaji ) wa zamani pale Mghahawani Kwake Food World tulivyokuwa tukimuita pia ndiyo Mwalimu wa Umafia ambao leo hii mnawasifia hawa akina Bin Kleb na Seif Magari.

Binafsi pamoja na Juma Nkamia kwa kushirikiana nae Kassim Dewji ( KD ) Mechi ya Simba SC na Ismaili FC Uwanja wa Uhuru (Shamba la Bibi) tulifanya Jambo moja la Kufuru na la Hatari lakini Mimi na Juma Nkamia kuna sehemu tulifika tukaogopa ila Kudadadeki zake Kassim Dewji aliuchukua Mzigo Mmoja hatari akaenda nao Uwanjani 'Kimafia' na Kushughulika nao Mwenyewe na kurudi ila 'Babu' alikosea Masharti na akaleta Mvua Kubwa japo Mshambuliaji Wetu Emanuel Gabriel alifunga Goli ila Mechi ililazimika Kuahirishwa kutokana na Uwanja Kujaa mno Maji.

Acheni tu tumetoka mbali na hii Simba SC ila Kassim Dewji si Mtu wa Kawaida na bado sijaona Mafia kama Yeye katika Mpira huu wa Tanzania.
 
Wewe ni chawa wa Kassim
 
Kwanza nitambue mchango wa KD hapo Simba amejitolea sana ila ukichunguza sana amejitolea kwa manufaa yake binafsi zaidi,yeye ndio amefaidika sana na Simba kuliko Simba ilivyonufaika nae!! Ameongoza Simba kipindi cha giza ambako wanachama na wapenzi na watanzania kiujumla walikuwa hawana uelewa zaidi ya propaganda za viongozi,yeye aliogopwa kuwa anafuga majini watu waliamini kuwa ukigombana nae unaishia kufa!!kama walivyokufa marehemu Juma aliekuwa mwenyekiti wa club aliepata ajali ya gari akitoka Dodoma kwenye kikao na waziri Kapuya ambae alikuwa anawapatanisha baada ya ugomvi wa mwenyekiti juma Salum na KD.

Khasim Dewji ni tapeli lililokubuhu alijimegea sehemu ya ardhi ya club akajenga jengo lake binafsi pale msimbazi kinyemela,amekuwa akizalisha na kuuza jezi za Simba toka miaka ya tisini bila kuinufaisha club ya Simba! Alijimilikisha jengo la club na kulikodisha kwa wafanyabiashara uku kodi zote akichukua yeye kwa zaidi ya miaka kumi na tano madai kuwa anaidai club pesa nyingi eti alikuwa akiikopa club!!

Haitoshi alikuwa anasajili yeye wachezaji na kufanya udanganyifu kwa kiasi cha pesa alichompa mchezaji kwa kuongeza pesa ili haidai club pesa nyingi zaidi, amewahi kujiweka pembeni mara kadhaa hasa kwenye uongozi wa Aden Rage na pia mwanzoni kwenye uongozi wa Dalali na Kaduguda hasa akibanwa kuhusu pesa za jengo la club.

Haliwahi kumshawishi ndugu yake MO Dewji waanzishe timu yao,wakaanzisha African Lyon ambayo MO alimkabidhi KD aiendeshe hakufanikiwa aliishia kumtapeli ndugu yake uyo ambae mpaka leo hawaivi vizuri, na KD ndie alikuwa akiendesha kampeini MO asiwe muekezaji hapo Simba maana alijua MO akiingia Simba timu itajiendesha ki weredi na mirija ya unyonyaji itazibwa,yeye ndie alikuwa akiwafadhili wakina mzee kilomoni kuvuruga mchakato wa uekezaji.

Nchi hii ukisikia mtu anaitwa mafia na sifa nyingine za kijinga ujue ni mwizi na mpigaji,toka MO Ameingia Simba na babra kuwa CEO mianya mingi imezibwa hasa kwenye pesa za usajili,uzalishaji wa jezi na pesa za majengo ya club ambayo KD alijimilikisha kinyemela,na pesa za kuhonga na urozi ambazo MO amekataa mara kadhaa kutoa pesa za ushirikina ambazo wajanja walikuwa wanachukua kwa kisingizio cha kutafuta ushindi.

wajanja wote ambao walikuwa wanaitumia simba kujinufaisha kwa sasa wako hoi na wengi wamesusa maana hakuna fedha za bure, najua ni ngumu kuwamaliza ila waelewe watanzania angalau hiki kizazi cha internet wanajua sana sayansi ya mpira na sio propaganda za kizamani,KD abadilike maana wanasimba wa leo sio wa miaka ya tisini.
 
Tatizo mmeamini uchawi zaidi kuliko ueledi zaidi , unamaanisha timu ikae inategemea tunguli na hiyo iwe sababu ya kumpigia magoti Kassim?
 
Asante kwa uchambuzi makini kabisa ,KD anapaswa kuelewa zama zimebadilika
 
Kipi msichoelewa hapo, Kassim Dewji na mm wap na wap, nawaambia nyie wajinga mnaotukana ambao mmeingia kwenye mpira juzi tu
Kichaa wewe,

Huyo kassim Tangu apokonywe tonge la Jezi amekuwa na hasira. Walikuwa hapo Simba Ila team haukuwahi kuwa na Eneo la kufanya hata Jogging. Leo chini ya CEO Barbra najua unajua kinachoendelea pale Bunju.

Huo uswahili ndio hatuutaki Simba, Yanga imepiga hatua Kwasababu ya kuachana na uswahili. Msitake kuturudisha nyumA tafadhali.
 
Mleta mada ni kichaa
 
Hizi takataka kila ukifikiri zimeisha unakuta zimejaa huku,huu upumbavu wa kuwategemea wahuni na waswahili watuletee maendeleo hatutakaa tupige hatua. Babra anapambania Simba isimame kama taasisi sio kama kikundi cha wahuni kama hao akina Kassim na the likes.Hao wahuni wanaleta Furaha za muda mfupi ila wanatupiga pakubwa na huwa wanakata pumzi na tm inaanza kufanya vibaya kama Kassim alivyofanya alivyokuwa katibu mkuu pumzi ikakata akakimbia. Babra anatosha wanaompinga ni wahuni,waswahili na wapigaji tu, sisi tunaoangalia miaka kumi ijayo tunamuombea kwa Mungu baba abaki simba.
 
NAKAZIA.
 
Upuuzi mtupu,,

Kassim dewj ndy waliouza Simba fainali ya CAF mwaka 1993.

Babbra anachukiwa na genge la upigaji Simba.
 
Haya mambo yafike wakati yaishe , watu washatoka huko mnapotaka kuwarudisha.

Simba lazima iendeshwe kisasa kulingana na mabadiliko yaliyofikiwa .

Sasa mnapoanza sijui nani ni mafia , uliambiwa tupo Sicily hapa .
Soka limebadilika sana , sajilini vizuri timu ifanye vizuri sasa ona wachezaji wengi tu pale kwa sasa ni maveteran unategemea nini..?

Kuanza kumlaumu mtendaji Barbara inaonekana kuna maslahi flani watu wamedhibitiwa sana.

Acheni haya mambo ya uswahili swahili kwenye soka , heshimuni taratibu za klabu ilizojiwekea pamoja ni viongozi wake.

Muhimu fanyeni usajili wa maana, wazee wengi kwenye timu hawana msaada.
 
Mchukue Kasim Dewji mkaanzishe timu yenu, upuuzi wake wa kihindi asilete wakati huu
 
Hoja za kichawichawi na utumwa wa fikra
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…